Dk Phillip Mpango Akataa Kuwa Waziri OmbaOmba......Asema Serikali Haipo Tayari Kukubali Ndoa Za Mashoga Kisa Misaada Ya WahisaniWAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango amesema hatua ya Serikali ya kukusanya kodi kwa nguvu kwa baadhi ya wafanyabiashara waliotorosha makontena bila kulipiwa ushuru, haikuwa lengo la kumkomoa mtu, bali ililenga kukusanya fedha za Serikali yenye lengo la kuifanya nchi iache utegemezi wa wahisani.

Waziri huyo ambaye jana alikutana na makundi mbalimbali ya wafanyabiashara ofisini kwake Dar es Salaam, alisema yeye kama waziri wa fedha asingependa kuwa waziri ombaomba kwa wahisani, ambao alidai baadhi yao wana masharti magumu, ambayo hayatekelezeki kwa maadili ya Watanzania.

“Nimewasindikiza wenzangu huko nje kuomba fedha sasa nimechoka, nataka kutembea kifua mbele, maana wana masharti magumu, wengine wanataka turuhusu homosexual (ndoa za jinsia moja), masharti haya kwa kweli yanakera sana,” alisema Dk Mpango ambaye katika serikali iliyopita alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango.

Dk Mpango aliongeza kuwa ili nchi isonge mbele, ni lazima ikusanye kodi ya kutosha; na jana aliahidi kuchukua hatua kadhaa, zitakazoiwezesha sekta binafsi kuwa mhimili wa kuimarisha uchumi wa nchi ili kufikia malengo ya kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye kipato cha kati.

Alisema Rais John Magufuli ni kiongozi ambaye akilala na kuamka, anawaza namna ambavyo atawahudumia wananchi wake, ambao wengi wako kwenye dimbwi la umaskini. 

Alisema Rais atafanikiwa tu, pale Serikali yake itakusanya kodi ya kutosha na kuwahudumia wananchi hao.

“Kuna minong’ono kwamba eti Serikali ya Awamu ya Tano inawanyanyasa wafanyabiashara wakubwa na kwamba hatua tulizochukua kukusanya kodi, ililenga kuwadhalilisha baadhi ya wafanyabiashara, hii sio kweli kabisa,” alisema Dk Mpango.

Dk Mpango alisema Serikali ya Awamu ya Tano, inatambua umuhimu wa wafanyabiashara, hivyo wizara yake itakuwa ya mwisho kuchukua hatua za kuwanyanyasa. 

“Nawahakikishia kwamba nina dhamira ya dhati ya kufanya kazi kwa kushirikiana na ninyi wafanyabiashara wakubwa na wadogo ili tutimize ndoto ya Rais,” alisema.

Alisema serikali yoyote duniani ni lazima ikusanye kodi, hivyo aliwahakikishia wafanyabiashara hao kuwa kama bado kuna wafanyabiashara wanaokwepa au hawataki kulipa kodi kwa mujibu wa sheria, serikali haitakuwa tayari kuwavumilia.

Dk Mpango alisema idadi ya watu wanaolipa kodi kwa sasa nchini bado wachache, hivyo aliwaagiza wafanyabiashara wote kujisajili wapatiwe Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN).

Pia, aliwataka waache tabia ya kufanya udanganyifu kwa kuwa na vitabu vingi vya utunzaji wa kumbukumbu za biashara. Aliwaagiza kuhakikisha wanatoa stakabadhi na suala hilo lisiwe hiyari.

“Tunajua kwamba mnatoa vitisho kwa wanunuzi kuwa kama wanataka risiti bei ni ya juu, hiki mnachofanya ni hatari kwa nchi,” alisema na kuwataka wote watumie mashine za EFD na serikali inaendelea na mpango wa kununua zingine ili wagawiwe bure.

Aliwataka kutoa taarifa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, kama kuna mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) au wa Halmashauri ya Wilaya, ambaye atadai hongo au atawanyanyasa wakati wa kudai kodi.

Katika kutekeleza hilo, aliwapatia namba zake pamoja na za Kamishna na kuwataka waache tabia ya kutoa rushwa ili wasilipe kodi.

 Dk Mpango alisema baada ya wafanyabiashara kufanya kikao na Rais Magufuli, Serikali imeunda kikosi kazi kushughulikia kero zote, zilizotolewa na Baraza la Biashara na mojawapo ni kufuta utiriri wa kodi ili kuwapa wepesi wawekezaji kufanya biashara nchini na kumpungumzia mzigo mkulima.
Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF