Breaking News: Matokeo Ya Mtihani Kidato Cha Nne -2015 Yametoka Jitazame/Mtazame Mwanao,Ndugu....Yatazame Hapa Ufaulu ni asilimia 67.91,Ufaulu Umeshuka asilimia 1.85,JIHUKUMU HAPA - LEKULE BLOG

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 18 February 2016

Breaking News: Matokeo Ya Mtihani Kidato Cha Nne -2015 Yametoka Jitazame/Mtazame Mwanao,Ndugu....Yatazame Hapa Ufaulu ni asilimia 67.91,Ufaulu Umeshuka asilimia 1.85,JIHUKUMU HAPABaraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2015 yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.
  
Msonde amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).
  
Amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwaasilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.
  
Aidha kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dkt Msonde amesema watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa 29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.
  
Kwa upade wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, Msonde amesema waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.
  
Aidha waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.
  
Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na wasichana 38,338 sawa na asilimia 19.63.
  
Amesema kwa upande wa ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule, ufaulu wa juu kabisa ni wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 77.63 wamefaulu huku ufaulu wa chini kabisa ukiwa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 16.76 wamefaulu.
  
Matokeo hayo yamepangwa katika mfumo wa madaraja (Division) badala ya ule wa wasatani wa alama (GPA) kama ambavyo iliagizwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi hivi karibuni.


Post a Comment
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.