Mkurugenzi Mkuu wa Blogu ya Wananchi, William Malecela ‘Le Mutuz’ , akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Blogu ya Wananchi, William Malecela ‘Le Mutuz’ , akionesha
kompyuta mpakato kwa wanahabari ambayo alianza kuitumia baada ya
kuanzisha blogu hiyo miaka mitatu iliyopita.
Mkurugenzi
Mkuu wa Blogu ya Wananchi, William Malecela ‘Le Mutuz’ (kushoto),
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu blogu hiyo
kutimiza miaka mitatu na semina itakayowakutanisha wasomi wasio na kazi
kuhusu namna ya kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Blogu ya Wananchi Media leo itaadhimisha miaka mitatu tangu
kuanzishwa kwake, sherehe itakayofanyi Hyatt Regency Kempisky zamani
Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa blogu hiyo,
Wiliam Malecela (Le Mutuz), alisema kuwa wameamua kufanya sherehe
kutokana na mafanikio waliyopata katika kipindi hicho, bendi ya muziki
wa kizazi kipya ya THT itatumbuiza.
Alisema
licha ya kesho(Leo) kufanya sherehe , leo(Jana) itakuwa na semina
maalumu ya vijana 300, ambao watakuwa pamoja na matajiri 6 vijana na
vijana watatu viongozi wa wa kitaifa kwa lengo la kubadilishana mawazo
na matajiri na viongozi hao, ambao wataeleza walivyopigana mpaka kufikia
walipo kimaisha.
Alisema
alianzisha blogu hiyo baada ya kuisajili kwa msajili wa makampuni
(Brela) 2012, ikianza kwa kutembelewa na watu 200 kwa siku lakini kwa
sasa inatembelewa na watu 70,000 mpaka 100,000 kwa siku kitu ambacho
anajivunia na kuwashukuru wadau.
Kampuni
hiyo ilianza kwa mtaji wa dola ya Marekani 500, ikiwa na usajili wa
makampuni wa Brela, na inatoa ajira kwa vijana 4 waliomaliza vyuo vikuu
nchini na ina ofisi yake katika jengo la Tancot House Sokoine Drive, Dar
es Salaam.
Alisema
katika miaka mitatu blogu imeweza kuwa na domain yake wenyewe ya
www.williammalecela.com na kuingia kwenye Facebook, Twitter, na
Instagram ambapo sasa inarushahabari sehemu mbalimbali kwa wakati mmoja
na kuweza kuwafikia watu hadi 500,000 kwa siku.
Alisema
mipango ya baadaye ni kuwekeza kwenye kampuni mpya ya African Swahili
Media Radio & Television ambayo tayari imeshapata leseni ya kufungua
radio na televisheni ambayo inatazamiwa kuwa hewani Aprili mwaka huu,
kituo cha radio kitakuwa Morogoro na televisheni Dar es Salaam,
anatarajia kutoa ajira zaidi angalau kwa vijana 10.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062
No comments:
Post a Comment