February 11 stori zilizoingia kwenye headlines katika soka la Uingereza ambalo linaaminika kuwa na mashabiki wengi wanaopenda Ligi hiyo, ni kuhusu winga wa zamani wa klabu ya Man City anayeichezea klabu ya Sunderland kwa sasa Adam Johnsonkuvunjiwa mkataba wake na klabu hiyo na wadhamini wake Adidas.
Klabu ya Sunderland imefikia maamuzi hayo baada ya winga huyo kukiri kuhusika kumrubuni kimapenzi msichana mwenye umri chini ya miaka 16, kitu ambacho ni kinyume cha sheria, winga huyo mwenye umri wa miaka 28 alikiri kosa la kumrubuni kwa njia ya mtandao (grooming) binti huyo ambae ni mwanafunzi, kukutana nae kumshika maungo yake na kumbusu.
Kosa hilo limefanya klabu yake ya Sunderland kuvunja mkataba nae lakini pia wadhamini wake Adidas wamevunja mkataba nae, kwa kukiri kosa hilo Adam Johnson huenda akahukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu jela na kama akikiri makosa yote huenda akafungwa miaka 14 jela. Adam Johnson ambaye kesi hiyo ilianza toka mwaka jana alijiunga na klabu ya Sunderland mwaka 2012 kwa dau la pound milioni 10 akitokea klabu ya Man City. Kesi hiyo itaendelea tena Ijumaa ya February 12.
No comments:
Post a Comment