ASSANGE KUJISALIMISHA IJUMAA MCHANA BAADA YA UAMUZI WA JOPO LA UMOJA WA MATAIFA - LEKULE

Breaking

6 Feb 2016

ASSANGE KUJISALIMISHA IJUMAA MCHANA BAADA YA UAMUZI WA JOPO LA UMOJA WA MATAIFA

Julian Assange, mwanzilishi wa mtandao wa habari za uchokonozi wa WikiLeaks
Julian Assange, mwanzilishi wa mtandao wa habari za uchokonozi wa WikiLeaks

Mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeak, Julian Assange, amesema atajisalimisha mwenyewe kwa polisi wa Uingereza siku ya Ijumaa, ikiwa jopo la umoja wa Mataifa litaamua kuwa hakuwa kizuizini, baada ya kutumia muda wa miaka mitatu akipewa hifadhi kwenye ubalozi wa Ecuador jijini London.
Assange amesema kuwa ikiwa umoja wa Mataifa utatangaza kuwa ameshindwa kesi dhidi ya Uingereza na Sweden, atajisalimisha mwenyewe majira ya mchana kwa maofisa wa polisi na kwamba kutakuwa hakuna haja zaidi ya kukata rufaa.Mwanzilishi huyo akaongeza kuwa ikiwa itaamuliwa vinginevyo na mahakama ikaona kulikuwa na ukiukwaji wa sheria, anatarajia kuona narejeshewa pasi yake ya kusafiria haraka sana na kufutwa kwa mipango mingine yoyote ya kumkamata.Assange amekuwa akipatiwa hifadhi kwenye ubalozi wa Ecuador toka mwaka 2102 katika jaribio lake la kukwepa kukamatwa na kusafirishwa kwenda Sweden kujibu mashtaka ya ubakaji, mashtaka ambayo mwenyewe amekana.
Mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeak, Julian Assange(Kushoto) akiwa na balozi wa Ecuador mjini London
Ecuador ilimpa hifadhi Assange lakini anakabiliwa na kukamatwa muda wowote atakapotoka na kukanyaga ardhi ya Uingereza ambapo polisi wamekuwa wakilinda nje ya ubalozi huo kwa muda wote.
Tofauti na kusafirishwa nchini Sweden, Assange anahofia pia kusafirishwa kwenda nchini Marekani ambako anakabiliwa na kesi ya kuvujisha maelfu ya nyaraka za siri za jeshi la Marekani kupitia mtandao wake.Assange alizindua mtandao wa WikiLeaks mwaka 2006 na harakati zake zilikuwa ni pamoja na kuchapisha nyaraka za siri za jeshi la Marekani zaidi ya laki 5 kuhusu vita ya Afghanistan na Iraq, huku nyaraka laki 2 na elfu 50 zilihusu mawasiliano ya wanadiplomasia wake.
Mtuhumiwa mkuu wa kuvujisha nyaraka hizo, mwanajeshi wa Marekani, Chelsea Manning alihukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kukiuka sheria ya usiri ya Marekani.

No comments: