Mbunge
wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amefunguka na kuonesha masikitiko yake kwa
kitendo cha serikali kushindwa kuleta Bungeni mpango wake wa maendeleo
wa miaka mitano.
Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook ameweka wazi jambo ambalo serikali inapaswa kufanya baada ya uchaguzi na kusema ni kuwasilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano.
"Shughuli
ya kwanza ya serikali baada ya uchaguzi ni kuwasilisha mpango wa
maendeleo wa miaka mitano ( kutafsiri ilani yake kwenda kwenye mpango wa
utekelezaji) . Bunge linapaswa kujadili na kuidhinisha Mpango wa
Maendeleo wa miaka 5 na kisha Mpango wa mwaka mmoja kuanza kutekeleza
Mpango huo wa miaka 5. Kwa mujibu wa Katiba ya JMT Ibara ya 63(3)(c),
Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 hutungiwa sheria kwa ajili ya
utekelezaji." Alisema Zitto Kabwe
"Leo
Serikali ya Rais John Magufuli ilipangiwa kuwasilisha Mpango huo wa
Maendeleo wa miaka 5. Imeshindwa. Imeleta mwelekeo wa Mpango. Haikuleta
sheria na Kamati ya Bajeti Imeleta maelezo yake kuhusu Mpango wa
Maendeleo wa mwaka mmoja ilhali hakuna Mpango wa Miaka 5.
"Mwenyekiti
Chenge alitaka wabunge wajadili kwa mujibu wa kanuni ya 94 ambayo
kimsingi ni Kanuni inayohusu Mpango wa mwaka mmoja. Serikali
imejichanganya. Uongozi wa Bunge umechanganyikiwa." Aliongeza Zitto Kabwe
Zitto Kabwe alimaliza kwa kusema kuwa ni aibu kubwa kwa serikali inayojinasibu kwa kauli ya "Hapa kazi tu"
"Bunge
linapaswa kuagiza Serikali ikalete Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 ili
uidhinishwe na utungiwe Sheria kabla ya kuanza kujadili mipango ya mwaka
mmoja mmoja.
"Ni
aibu kubwa kwa Serikali ya #HapaKaziTu kushindwa kuleta Bungeni
Mpango wake wa Maendeleo wa miaka 5 na hata ule wa mwaka wake wa kwanza.
Itapangaje bajeti zake? Itatekeleza vipi ilani yake? Kuongoza nchi sio kutumbua majipu tu, ni kuendesha nchi." Alimaliza Zitto Kabwe.
No comments:
Post a Comment