Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salaam
(DAWASCO) Mhakndisi Cypian Luhemeja akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya
Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Mbogo Mfutakamba ,wakielekea katika kikao
cha Unongozi na wafanyakazi wa DAWASCO kilichofanyika makao makuu y a
shirika hilo.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu w Shirika la Maji safi na Maji taka Dar
es Salaam,DAWASCO,Bi,Joy Chidosa akifanya utamburisho katika kikao
hicho.
Baadhi ya Mameneja wa vitengo mbalimbali katika Shirika la Maji
safi na Maji taka jijini Dar es Salaam DAWASCO ,wakiwa katika kikao
hicho.
Afisa Mtendaji mkuu wa DAWASCO,Mhandisi Cyprian Luhemeja
akifurahia jambo na katibu mkuu wa wizara ya maji na umwagiliai Mhandisi
,Mbogo Mfutakamba.
Afisa Mtendaji mkuu wa DAWASCO,Mhandisi Cyprian Luhemeja
akizungumza wakati wa kikao cha wafanyakazi kilicho fanyika makao makuu
ya ofisi za Dawasco.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagliaji,Mhandisi Mbogo
Mfutakamba akizungumza na wafanyakazi wa DAWASCO wakati wa kikao
kilichofanyika makao makuu ya shirika hilo .
Baadhi ya wafanyakazi wa DAWASCO wakiliombea dua shirika hilo ili
liweze kutimiza malengo yake ya kutoa huduma ya maji safi na maji taka
kwa usalama kwa wakazi wa miji ya Dar es Salaam,Kibaha na Bagamoyo.
Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini aliyekuwa jijini Dar es Salaam.
WIZARA ya maji na umwagiliaji, imesema inaridhishwa na kasi ya
utekelezaji wa mipango ya usambazaji wa huduma za maji, inayofanywa na
shirika la majisafi na majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) na kutoa
rai kwa watumishi wa shirika hilo kushirikiana ili kufikia malengo ya
utoaji wa huduma kwa wananchi.
Hayo yalisemwa jana na katibu mkuu wa wizara hiyo mhandisi Mbogo
Futakamba, alipokuwa akiwahutubia wafanyakazi wa DAWASCO, katika makao
makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Futakamba, alisema kasi ya utoaji wa huduma bora za maji
kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, imepunguza malalamiko mengi ya
wananchi, na kwamba serikali imeanza kupata matumaini makubwa na kujenga
imani kwa shirika hilo kwa kufanikisha malengo makuu ya usambazaji wa
huduma hiyo kwa wananchi.
Aidha alisema kwa kiwango kikubwa wizara ya maji na umwagiliaji
kwa sasa inajivunia kwa kazi nzuri iliyofanywa na shirika hilo, hasa kwa
kuzingatia kuwa DAWASCO ndio jicho la wizara kutokana na wingi wa
wananchi wanaohitaji huduma za maji zinazosambazwa na shirika hilo.
“Nimeona jitihada zenu, nimependa jinsi mnavyofanya kazi kama
timu, naomba muwe na uaminifu mkubwa sana katika kazi, kuweni
wawajibikaji ili wananchi wapate huduma ya maji”, alisema mhandisi
Futakamba.
Katika hatua nyingine katibu mkuu huyo alipongeza juhudi kubwa
zilizofanywa na shirika hilo za kupunguza kiwango cha upotevu wa maji
pamoja na kudhibiti wizi wa maji, ambavyo vimekuwa kikwazo
kinachochochea malalamiko ya wananchi kwa shirika hilo.
Awali akitoa taarifa ya shirika hilo, afisa mtendaji mkuu wa
DAWASCO, mhandisi Cyprian Luhemeja, alisema shirika hilo limefanikiwa
kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji, baada ya kuongeza uzalishaji
kutoka mita za ujazo 7,834,234 hadi mita za ujazo 8,421,370 kati ya
mwezi Mei hadi Novemba 2015.
Alizitaja sababu za mafanikio ya ongezeko la kiwango cha maji ni
pamoja na udhibiti wa upotevu wa maji katika bomba kubwa, kufanya
matengenezo ya tahadhari, maboresho ya maslahi ya wafanyakazi na
kuboreshwa kwa kitengo cha upotevu wa maji.
Mhandisi Luhemeja alibainisha kuwa DAWASCO, imefanikiwa kufunga
dira katika maungio ya maji, kuziba maeneo yanayovujisha maji kwa
wakati, kupambana na wezi wa maji, kuhakiki ufanisi wa dira za maji,
kusajili maboza ya wauzaji maji na kuboresha usomaji wa dira, ambavyo
viliwezesha kupunguza kiwango cha maji yanayopotea kutoka asilimia 62
hadi 45, kati ya mwezi Mei mpaka Novemba 2015.
Aliongeza kuwa mafanikio ya utekelezaji wa mipango ya uboreshaji
wa huduma za maji yaliwezesha shirika hilo la DAWASCO, kuongeza
makusanyo ya mapato kutoka shilingi bilioni 2.9 hadi kufikia bilioni 6.2
kati ya mwezi Mei hadi Novemba 2015.
Wakati huo huo shirika hilo limeanza kutekeleza agizo la serikali
linaloitaka DAWASCO, kuongeza idadi ya wateja wake hadi kufikia milioni
moja, katika jiji la Dar es Salaam, miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani,
hadi kufikia mwezi Juni 2016.
Katika utekelezaji wa agizo hilo DAWASCO iko katika utekelezaji wa
Maagizo ya serikali ya kuhakikisha wananchi waishio katika Jiji la Dar s
salaam, Miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani Pwani wanaunganishiwa Maji
ifikapo Julai 2016. Katika kutekeleza agizo hilo Dawasco imejipanga
katika awamu kuu NNE (4)
1. Awamu ya kwanza itawahusu wateja wote walioko katika
maeneo ambayo kwa sasa yanapata maji na kuna miundo mbinu ya mabomba
karibu.
2. Awamu ya Pili itahusu maeneo ambayo yamepitiwa na mabomba
makubwa ya Maji jirani lakini wananchi wake hawana maji kwa sababu ya
kukosekana kwa miundo mbinu ya usambazaji.
3.
Awamu ya Tatu itahusisha maeneo yote yaliyopitiwa na mradi maarufu wa
Mabomba ya Kichina, Maunganisho katika awamu hii yataanza baada ya
kukamilika kwa Miradi ya Ruvu Chini na Ruvu Juu,
4. Awamu ya Nne itaanza katika maeneo yote ambayo kwa sasa
hakuna miundo mbinu ya Maji na yako mbali kutoka katika mabomba makubwa .
Gharama ya kuunganishiwa huduma ya Majisafi ni Tsh 200,000 kwa
wateja wadogo (Domestic Customers)na Tsh 400,000 kwa wateja wakubwa
(Corporate Customers).
No comments:
Post a Comment