WAZIRI wa
Maji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge leo amekutana na mabalozi wa Misri na
Denmark kwa nyakati tofauti ofisini kwake, Makao Makuu ya Wizara ya Maji
na Umwagiliaji, Ubungo Maji.
Huu ni mwendelezo wa mazungumzo ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Mhe. Inj. Lwenge na washirika wa maendeleo na wadau wa Sekta ya Maji ya
kuweka mikakati ya kuinua na kuendeleza Sekta ya Maji nchini, mara baada
ya juzi pia kukutana na Balozi wa Ubelgiji, Mhe, Paul Cartier.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akizungumza na Balozi wa Misri, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa kwenye mazungumzo
na Balozi wa Misri, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf na Mkurugenzi
wa Rasilimali za Maji, Hamza Sadiki.
Balozi wa Misri, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf akimpa zawadi Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge.
Balozi
wa Denmark, Mhe. Einar H. Jensen akisaini Kitabu cha Wageni, kwenye
ofisi ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji, akiwa na msaidizi wake, Kansela
wa Uchumi na Usimamizi wa Fedha za Umma , Mette Melson.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa na Balozi wa Denmark, Mhe. Einar H. Jensen.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge, Balozi wa Denmark,
Mhe. Einar H. Jensen na Mkurugenzi wa Maji Mijini, Inj. Dkt. Justus
Rwetabula.
No comments:
Post a Comment