Waziri Mkuu Atoa ONYO Kali Kwa Madaktari Wanaotoa Mimba Wanawake.....Aapa Kuwafukuza Kazi Na Kuwafunga Jela - LEKULE

Breaking

6 Jan 2016

Waziri Mkuu Atoa ONYO Kali Kwa Madaktari Wanaotoa Mimba Wanawake.....Aapa Kuwafukuza Kazi Na Kuwafunga Jela


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia Josephine John  ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa matibabu. Alikuwa katika ziara ya mkoa huo Januari5, 2016.

********

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya Madaktari vinara wa Hospitali ya Rufaa ya Songea ambao wanasifika kwa kufanya biashara ya kutoa mimba wanawake na wanafunzi kuacha tabia mara moja,lasivyo  atawafukuza kazi na kuwafunga jela.

Waziri Mkuu alitoa onyo hilo jana wakati alipotembelea Hospitali hiyo na kuzungumza na watumishi kwa lengo la kuwasisitiza kutoa huduma bora kwa wagonjwa,ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 mkoani Ruvuma.

Alisema Hospitali ya mkoa huo inasifika kwa kutoa mimba wanawake na kuwalaza wagonjwa wao wodi namba 5, kitendo ambacho serikali haikuruhusu wala haikubaliani nacho.

"Naomba mkuu wa mkoa fanya ziara ya kushtukiza katika wodi namba 5 utakuta wanawake wametolewa mimba, wakiwemo wanafunzi na kisha madaktati hao wanatumia wodi zetu kuwalaza wagonjwa wao waliowatoa mimba.Ni marufuku na nitawachukulia hatua kwani majina ya madaktari hao ninayo," alisisitiza majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Dr. Daniel Malekela na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dr. Phils Nyimbi kuwafuatilia madaktari wanaojihusisha na vitendo hivyo na kutoa taarifa ili wachukuliwe hatua kali.

Pia, alimuagiza mganga mkuu Dkt Daniel Malekela kuondoa duka lake lililo jirani na hospitali hiyo ili kuondo hisia kwamba dawa zinaibiwa na kupelekwa kwenye maduka ya watumishi.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Thabiti Mwabungu na kulia ni Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na bibi Antonia Moyo ambaye alikuwa akipata matibabu katika chumba maalum cha waze katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma wakati alipoitembelea hositali hiyo akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Thabiti Mwabungu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,akimsalimia mtoto Flora Mapunda (1) ambaye amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambayo  Waziri Mkuu aliitembelea na  kuzungumza na watumishi  akiwa ktika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.

No comments: