Wanasheria Waikosoa ZEC Kufuta Uchaguzi Zanzibar....Wamtaka Rais Magufuli Aingile Kati Kuokoa JahaziWanasheria nchini wamemtaka Rais John Magufuli ingilie kati sakata la Zanzibar kwa sababu sintofahamu inayoendelea kutokea visiwani humo ni aibu ya Tanzania mbele ya Jumuiya ya Kimataifa.

Wakizungumza jana katika mdahalo ulioandaliwa na Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) kujadili changamoto za kisheria zilizojitokeza katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 25 mwaka 2015, wanasheria hao walisema Rais Magufuli anaweza kutumia nafasi yake kumaliza sintofahamu hiyo.

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman alisema kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar kumekiuka Katiba na sheria mbalimbali za uchaguzi zinazosimamia uchaguzi.

“Ingawa haya yanatokea Zanzibar, lakini ni suala la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunamtaka Rais Magufuli katika kutumbua majipu alione na hili la Zanzibar tunataka alipasue kabisa.”

Aliongeza kuwa, “kuendelea kutembea nalo linakuwa mzigo mkubwa, kwa hiyo tunamtaka kulipasua ili kutua hilo zigo.”

Othman alisema hakuna sheria yoyote inayompa mamlaka mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kufuta uchaguzi.

Alisema hata vifungu alivyovitumia Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha wakati anatangaza kufuta uchaguzi, vinazungumzia mambo mengine kabisa.

“Ni vema Rais Shein (Ali Mohamed) akajiuzulu kwa sababu yeye ni sehemu ya tatizo la Zanzibar. Hawezi kuendelea kugombea wakati yeye ndiye aliyesababisha mkwamo huo wa kisiasa,” alisema mwanasheria huyo.

Wakili Fatma Karume ambaye pia ni mtoto wa rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume alisema kuna haja ya kubadilisha kifungu cha 119 (10) kinachotaja sifa za mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi kwamba anatakiwa kuwa jaji wa Mahakama Kuu au mtu yoyote mwenye kuheshimika.

“Ni jambo la kushangaza kabisa, yaani Jecha anapewa uenyekiti wa Tume wakati hajui mambo ya kisheria halafu makamu wake ndiyo jaji. Hapa kuna tatizo na amewekwa hapo kwa ajili ya kulinda maslahi ya watu,” alidai wakili huyo.

Fatma alisema hakushangazwa na kitendo cha wanasheria kushindwa kwenda mahakamani kufungua kesi ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi kwa sababu anajua hawana imani na mahakama. Alisema yule aliyemteua Jecha (Rais Shein) ndiye aliyewateua pia majaji.

Mwakilishi wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jussa alisema Jecha ni kada wa CCM, hivyo hafai kuongoza Tume hiyo kwa sababu anaonyesha maslahi yake wazi wazi kwa chama hicho.

“Katika uchaguzi wa mwaka 2010, Jecha aligombea katika jimbo la Amani kupitia CCM akashindwa. Shein akaona amteue kuwa mwenyekiti wa ZEC ili kulinda maslahi yake.”

Jecha alitangaza kufuta uchaguzi huo wa rais, wawakilishi na madiwani visiwani humo akisema kanuni na taratibu zilikiukwa.

Uchaguzi huo kwa sasa umepangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu.
Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF