Wakati
muda wa `mapumziko’ ya bomoabomoa ukimalizika leo huku jaribio la
kupata zuio la muda likiwa limewekwa kiporo, wakazi wa Jangwani ambako
nyumba zitaanza kubomolewa leo, jana waliweka mabango barabarani
yanayotuma ujumbe wa aina mbalimbali kwa Rais John Magufuli.
Bomoabomoa
hiyo ilianza Desemba mwaka jana likilenga nyumba zilizojengwa kwenye
Bonde la Mto Msimbazi, lakini lilisitishwa kwa siku 14 na Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi hadi Januari 5,
mwaka huu kuwapa nafasi wakazi kuondoka kwa hiari yao kuokoa mali zao.
Wakazi
wa Jangwani walitumia mwanya huo wa kusitisha ubomoaji, kufungua kesi
Mahakama ya Ardhi kupinga kuondolewa maeneo hayo bila ya kupatiwa sehemu
nyingine na kuwasilisha ombi za zuio la ubomoaji, lakini chombo hicho
cha sheria kilikataa kubariki mambo hayo ya kutaka sitisho la bomoabomoa
liendelee wakati kesi ikiendelea mahakamani.
Wakati
wawakilishi wa wakazi hao wakiwa mahakamani katikati ya jiji, watumishi
wa halmashauri za jiji waliendelea kuweka alama nyumba zinazotakiwa
kubomolewa wakiwa wamesindikizwa na ulinzi mkali wa polisi.
Hakukuwepo
na wakazi waliojitokeza kuzuia uwekaji alama hiyo ya “X” inayotaarifu
kuwapo kwa ubomoaji, lakini mabango ya maboksi yaliyosimikwa kwenye
vifusi na maeneo mengine ya jangwani, yanatosha kuelezea hisia za wakazi
hao wanaoishi maeneo ambayo yametangazwa kuwa hatarishi.
No comments:
Post a Comment