Mkurugenzi Mtendaji wa Adidas, Herbert Hainer.
Wadhamini
wa Manchester United ambao ndiyo wanaoitengenezea klabu hiyo jezi,
Adidas wametoa maoni yao kuhusu mwenendo wa klabu hiyo na kusema kuwa
hawafurahishwi na aina ya uchezaji ya klabu hiyo ambayo wanaamini
haiwavutii mashabiki wa soka.
Kampuni
hiyo ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Ujerumani ambayo imeingia
mkataba na Manchester United wa miaka 10 wenye thamani ya Pauni Milioni
750 wameyasema hayo kupitia Mkurugenzi Mtendaji wa Adidas, Herbert
Hainer kuwa aina ya uchezaji wa Man United sio ambao wao wamekuwa
wakiutaka.
Alisema
licha ya kuwa katika kipindi kigumu lakini wanamatumaini klabu hiyo
itarudi katika ubora wake wa awali na licha ya kuwa na kipindi kigumu
lakini bado kampuni hiyo imekuwa na mauzo mazuri ya jezi za Man United
jambo ambalo lilikuwa hawalitegemei.
“Biashara
na Manchester United inakwenda vizuri, tunauza t-sherti zaidi ya
tulivyofikiria tunaridhishwa na hilo licha ya kuwa hatupendezwi na mfumo
ambao Man United wanacheza sio ambao sisi tunataka kuuona,” alisema
Hainer.
Manchester
United kwa sasa imekuwa katika kipindi ambacho kimekuwa hakiwaridhishi
mashabiki wengi wa klabu hiyo kutokana na aina ya matokeo ambayo imekuwa
ikiyapata ambapo katika michezo 15 imeyopita imefanikiwa kupata magoli
12 pekee hali inayopelekea mashabiki kadhaa kutaka kocha wa klabu hiyo,
Louis Van Gaal kutimuliwa kazi.
No comments:
Post a Comment