Vladmir Putin, rais wa Urusi
Wizara ya
Fedha ya Marekani imeiambia BBC kuwa rais wa Urusi Vladmir Putini
anakula rushwa.Tayari serikali ya Marekani imeshawawekea vikwazo
wasaidizi wa rais Putin na inaonekana ni mara ya kwanza kwa kumhusisha
moja kwa moja rais huyo na rushwa.
Msemaji wa wa rais huyo Urusi ameaiambia BBC hakuna maswali jambo lolote linapaswa kujibiwa kwa sababu ni wa kutunga.
Tuhuma
hizi zinakuja siku chache ambapo hivi majuzi tume ya uchunguzi ya
Uingereza iliyokuwa ikichunguza mauaji ya jasusi wa zamani wa Urusi
Alexander Litvinesko lilimtuhumu pia Putin kuwa huenda alitoa amri ya
kuuawa kwa jasusi huyo.
Litvinenko aliyekuwa akifanya kazi katika idara ya usalama ya urusi aliuawa kwa sumu ya polonium mjini London mwaka 2006.
Adam
Szubin anayesimamia vikwazo vya Wizara ya fedha vya Marekani amekiambia
kipindi cha Palorama cha BBC kuwa rais wa Urusi ni mla rushwa na hilo
lilifahamamika na serikali ya Marekani miaka mingi iliyopita.
"Tumemwona
akiwaneemesha marafiki zake na watu wake wa karibu na kuwakandamiza
wale ambao sio marafiki wake kwa kutumia rasilimali za taifa kama
utajiri wa nishati au mikataba baina yao na serikali amekuwa akitoa
maagizo iwanufaishe wale ambao anaamini watamnufaisha na kuwatenga wale
wasiomnufaisha. Kwangu mimi hiyo hiyo ni sura ya rushwa."
Maafisa
wengine wa Marekani waliogoma kuhojiwa kuhusu utajiri anaodaiwa kuwa nao
Putin ambaye na Szubin pekee aliyekubali kushiriki kwenye uchuguzi huo
uliofanywa na kipindi cha Panorama hata hivyo alikataa kutoa maoni yake
kuhusu ripoti ya siri ya Shirika la kijasusi la CIA iliyotolewa mwaka
207 kuhusu utajiri wa Putin unaofikia dola bilion 40.
Mwaka
2008 Putin Mwenyewe alizielezea tuhuma kwamba ni ana utajiri mkubwa kuwa
ni propaganda na hazina maana.Kuhusu tuhuma hizi za Rushwa Putin
alikataa kuhojiwa na kipindi hicho cha Panorama.
No comments:
Post a Comment