MBWANA SAMATA & AUBAMEYANG WACHEZAJI BORA AFRICA,LIST YA WASHINDI WENGINE WA TUZO ZA CAF WAKO HAPO - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Friday, 8 January 2016

MBWANA SAMATA & AUBAMEYANG WACHEZAJI BORA AFRICA,LIST YA WASHINDI WENGINE WA TUZO ZA CAF WAKO HAPO

Usiku wa January ndio siku ambayo watanzania na Afrika kwa ujumla walikuwa wakiisubiria kwa hamu. Kwa upande wa Tanzania huo ulikuwa ni siku wa kumshuhudia mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekpiga na klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta akiwa kasimama jukwaa moja na mastaa wengine wa soka wa Afrika katika utowaji wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika na mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wa ndani ya Afrika.
CYI7119WcAAt0ov
Mbwana Samatta ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wanaocheza Ligi ya ndani, wakati Pierre Emerick Aubemeyang kutokea Gabon katangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ujumla, Aubemeyang anakipiga katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Hii ndio list ya washindi wa tuzo hizo kwa mwaka 2015
  • Timu bora ya taifa kwa mwaka Ivory Coast
  • Timu bora ya taifa ya wanawake Cameroon)
  • Mchezaji mwenye uungwana (Fair Play) Allez Casa wa Senegal
  • Klabu bora ya mwaka TP MAZEMBE
  • Mchezaji bora chipukizi Etebo Oghenakoro
  • Mchezaji bora kijana Victor Osimhen wa Nigeria
  • Kocha bora wa mwaka ni Herve Renard mfaransa ambaye alikuwa kocha wa Ivory Coast
  • Mchezaji bora wa kike Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon
  • Refa bora wa mwaka ni Papa Bakary Gassama kutoka Gambia
1qv
1q
Samatta na Aubemeyang wakiwa pamoja dakika chache kabla ya kutangazwa mshindi.
Post a Comment