UFUNGUZI WA JENGO LA WAGONJWA WA NJE HOSPITALI YA KIVUNGE KASKAZINI UNGUJA

 Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Afya na Wananchi waliohudhuria katika sherehe za Ufunguzi wa Jengo la Hospitali ya Kivunge kwa Wagonjwa wa nje Wilaya ya kaskazini A,Mkoa wa Kaskazini Unguja lililojengwa kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali (HIPZ) kutoka Uingereza ikiwa ni katika shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe  kufungua Jengo la Wagonjwa wa Nje Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja lililojengwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali kutoka Uingereza (HIPZ) ikiwa ni katika shamra shamra za Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 (wa pili kushoto) Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo Jecha
  Viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wananchi mbali mbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini akitoa hutuba ya ufunguzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja leo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar
 Meneja Mipango wa Shirika lisilolakiserikali  kutoka Nchini Uingereza (HIPZ) Bibi Pamela Allard akitoa salamu zake wakati wa ufunguzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja leo lililofunguliwa naWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini ,kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame (kushoto) pamoja na Viongozi wa Wizara ya Afya wakiangalia Uodhoreshaji majina kwa wagonjwa wanaofika Hospitali kwa njia ya Mtandao baada ya kufungua Jengo la Wagonjwa wa Nje Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja leo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, sherehe hizi ni katika shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52,(wa pili kushoto) Dr,Alexander Vogt wa kujitolea wa Shirika la HIPZ kutoka Uingereza
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini (kushoto) akimsalimia Mtoto aliyefika kupima Nazna Ali Silima,miezi 5 uzito kilo 7.3 katika Hospitali ya Kivunge wagojwa wa nje,baada ya kifungua Hospitali hiyo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali (HIPZ) kutoka Uingereza,(katikati) Dkt.Tamim Hamad Said Daktari Dhamana Hospitali ya Kivunge na Muuguzi Filonema Raumond Woga 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kufungua Jengo la Wagonjwa wa Nje Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja,katika shamra shamra za Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 (wa pili kushoto) Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo Jecha
 Wawakilishi wa Mashirika ya Misaada ya kimaendeleo  ambayo yamesaidia vifaa mbali mbali wakitoa salamu zao wakati wa ufunguzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja leo lililofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini ,kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini akitoa hutuba ya ufunguzi waJengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja leo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, jengo lililojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la (HIPZ) kutoka nchini Uingereza ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar (kulia) Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt>Saleh Mohamed Jidawi na Naibu Waziri wa Afya mahmoud Thabiti KomboJecha
 Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alipokuwa akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini kutoa hutuba ya ufunguzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja leo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar
 Baadhi ya Viongozi wa Serikali na mashirika ya kimaendeleo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini akitoa hutuba ya ufunguzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja leo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini akipokea Kadi ya Mfuko wa Taifa wa Afya Kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo Bw,Michael Mhando,kadi hiyo imetolewa kwa ajili ya Mzee Makame Mjombo wa Gamba mweye umri wa miaka 140,wakati wa sherehe za ufunguzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A.Unguja leolililofunguliwa kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Ikulu, ZNZ
 
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                                                 9.1.2016
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa hatua za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba za kuimarisha huduma za afya za vijijini ni miongoni mwa utekelezaji wa shabaha ya Mapinduzi ya mwaka 1964 ya kuzifikisha huduma bora za afya hadi vijijini kwa nia ile ile ya waasisi wa Mapinduzi.
Dk. Shein aliyasema hayo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, mara baada ya kulifungua jengo la wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Kivunge, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katika hotuba hiyo, Dk. Shein alisema kuwa  huduma bora za afya kwa wananchi wote bila ya ubaguzi ni miongoni mwa malengo ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambapo Chama cha ASP kilichoongoza Mapinduzi hayo katika manifesto yake, kiliweka bayana azma yake ya kutoa huduma za afya bure bila ya ubaguzi wakati kitakaposhika hatamu za Serikali.
Dk. Shein alisema kuwa jitihada kubwa zimefanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kipindi cha miaka 52 ya Mapinduzi katika kuimarisha huduma za afya kwa kutambua kwamba afya bora ni muhimu kwa wananchi ili waweze kuishi vyema katika kazi ya kuleta maendeleo ya nchi yao.
Alisema kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika utekelezaji wa mipango na mikakati ya kuiendeleza sekta ya afya nchini kupitia vitengo na programu mbali mbali zinazoendeleshwa na Serikali kwa ushirkiano na Washirika wa Maendeleo.
“Nyote ni mashahidi wa kuimarika kwa huduma za afya katika hospitali na vituo vytetu vyote va afya... Aidha, kuna ongezeko kubwa la vituo vya afya vya daraja mbali mbali kiasi kwamba hivi sasa wananchi wa Zanzibar hawawezi kwenda zaidi ya kilomita tano bila ya kukuta kituo cha afya”,alisema Dk. Shein.
Akieleza historia ya huduma za afya katika Mkoa wa Kaskani Unguja, Dk. Shein alisema kuwa kabla ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 katika Mkoa huo kulikuwa na vituo viwili tu vya afya ambavyo vilikuwepo huko Mkokotoni na Chaani.
Alisema kuwa katika kipindi cha miaka 52 ya Mapinduzi Mkoa huo hivi sasa una vituo vya afya 26 ambapo vituo 18 ni vya daraja la kwanza na 7 ni vya daraja la pili pia, kuna hospitali ya Koteji ya Kivunge ambayo lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba ni kuipandisha daraja kuwa hospitali ya Wilaya.
Dk. Shein alisema kuwa lengo la mradi huo ulioanza mwaka 2012 ni kuziimarisha huduma za afya katika hospitali zote za Koteji ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali kuu ya Mnazi mmoja.
Aidha, Dk. Shein alisema kuwa Serrikali imekusudia kuzisogeza huduma za afya kuwa karibu zaidi na wananchi ikiwa ni pamoja na huduma za upasuaji kwa kinamama wajawazito, huduma za uchunguzi kama vile za maabara, “X-ray” na “Ultra-sound”.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa shukurani za dhati kwa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Uingereza HIPZ, UNICEF na ROTARY Club kwa kuiunga mkono Serikali katika lengo la kuiimarisha hospitali hiyo.
Dk. Shein alisema kuwa huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo zimeimarika sana baada ya Serikali kupitia Wizara ya Afya kuongeza wafanyakazi, vifaa vya uchunguzi wa maradhi na kuongeza aina za huduma zinzotolewa katika hospitali hiyo.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuwahimiza wazazi juu ya umuhimu wa kwenda kujifungulia hospitali na kuhudhuria kliniki ili kupima na kupatiwa ushauri pamoja na kuhakikisha watoto wanapelekwa vituoni kupatiwa chanjo kwa kuzingatia kampeni ya chankji kwa watoto zinazoendeleshwa na Wizara ya Afya.
“Serikali itaendelea kuzipatia ufumbuzi changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya afya kwa lengo la kuwapatia huduma bora za afya wananchi wote mjini na vijijini”,alisema Dk. Shein.
Aidha, Dk. Shein alitoa wito kwa wananchi wote kuendelea kusherehekea maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa amani na utulivu.
Nae Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo aliwaeleza wananchi waliohudhuria uzinduzi wa hopaitali hiyo kuwa hatua hizo ni miongoni mwa ahadi za Dk. Shein kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambazo ameziahadi na sasa anaendelea kuzitekeleza huku akitoa shukurani kwa washirika wa maendeleo yakiwemo Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mohemmed Saleh Jidawi alisema kuwa  juhudi mbali mbali zinaendelea kuchukuliwa na Serikali chini ya uongozi wa Dk. Shein katika kuhakikisha Hospitali za Koteji kuwa za Wilaya na kueleza kuwa gharama za ujenzi huo ni milioni 461 chini ya ufadhili kutoka kwa Shirika la HIPZ.
Dk. Jidawi alisema kuwa lengo ni kuhakikisha hospitali hiyo inakuwa ya Wilaya na kulipongeza Shirika la HIPZ kwa kuendelea na juhudi zake katika kuiimarisha hospitali ya Kivunge kama ilivyofanya kwa hospitali ya Makunduchi.
Alisema kuwa hospitali hiyo ina uwezo wa kupokea wagonjwa 120 hadi 140 kwa siku mbapo pia hopsitali hiyo itafanya kazi kwa masaa 24 huku akieleza kuwa hospitali hiyo inatumia mfumo wa kisasa wa kuwaorodhosha wagonjwa kwa njia ya Kompyuta kwa lengo la kupunguza kupotea kwa kumbukumbu.
Nao Washirika wa Maendeleo wakiwemo wawakilishi wa HIPZ, UNICEF,ROTARY CLUB pamoja na uongozi wa Mfuko Taifa wa Bima za Afya waliahidi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kuiimarisha zaidi huduma za afya hapa nchini ikiwa ni pamoja na kukiendeleza kituo hicho cha afya ili kitoehuduma bora kwa wananchi.
Aidha, washirika hao walieleza kuwa kituo hicho kitakuwa ni mkombozi kwa akina mama na kutoa shukurani kwa mashirikiano wanayoyapata kutoka kwa uongozi wa Wizara hiyo.
Viongozi mbali mbali wa vyama na serikali pamoja na mamia ya  wananchi walijitokeza katika hafla hiyo.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar


Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF