Mamlaka
ya Mapato ya Tanzania (TRA) imesema imeongeza muda kwa usajili wa
vyombo vya usafiri vya Pikipiki za magurudumu mawili na matatu mpaka
Februari Mosi mwaka 2016.
Hayo
yamesemwa leo na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata
alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika kikao chake cha
kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi, Kaimu Kamishna Mkuu
amesema wameamua kuongeza muda wa zoezi la usajili wa pikipiki ili
kuiwapa nafasi wale ambao bado hawajasajili.
“
Natoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya pikipiki kusajili vyombo vyao
mapema ili wasipatwe na adha itakayojitokeza baada ya muda uliotolewa
kumalizika ” Alisema Kaimu Kamishna Kidata.
Ameongeza
kuwa zoezi hilo lilikumbwa na changamoto kadhaa zilizowalazimu kuongeza
muda mara mbili, ambazo ni umbali wa vituo vya usajili na makazi ya
wamiliki wa pikipiki hasa mikoani,pamoja na upotevu wa nyaraka za
kununulia pikipiki.
Aidha
Kaimu Kamishna Alphayo Kidata ameomba wananchi kufungua ukurasa mpya wa
ushirikiano na Mamlaka ili kutimiza azimio la Serikali ya Awamu ya
Tano ya kulijenga taifa kwa kufanya kazi na hasa kulipa kodi stahiki
zinazoleta mapato yanayowezesha maendeleo katika taifa letu.
Zoezi
la usajili wa pikipiki lilianzishwa kwa lengo la kurahisisha ukusanyaji
wa mapato kutoka katika vyombo hivyo, zoezi hili lilipangwa kukamilika
tangu Desemba 31 2015 lakini ikaonekana wengi hawakusajili pikipiki zao
hivyo basi Mamlaka imetoa mwezi mmoja mpaka Februari Mosi 2016 kwa wenye
Pikipiki kusajili.
No comments:
Post a Comment