Rais Hassan Rouhani katika mkutano na waandishi wa habari Tehran. (Jumapili 17.01.2016)
Rais
Hassan Rouhani amesema Jumapili (17.01.2016) wale waliokuwa na mashaka
ambao walionya makubaliano ya nyuklia na mataifa yenye nguvu hayatokuwa
na manufaa kwa Iran "wote wamethibitishiwa kuwa walikuwa sio sahihi.
Rouhani
amewaambia waandishi wa habari mjini Tehran kwamba "masaa machache tu "
baada ya kuanza kutekelezwa kwa makubaliano hayo ya nyuklia na
kuondolewa kwa vikwazo "njia 1,000 za mikopo zimefunguliwa na benki
mbali mbali."
Amesisitiza
kwamba makubaliano hayo sasa yatarahisisha kampuni za Iran kufanya kazi
baada ya kutengwa kwa miaka mingi katika mfumo wa fedha wa kimataifa.
Rais huyo
amesema "leo tuko katika hali ambapo kwayo tunaweza kuwa na mawasiliano
ya kisiasa,kiuchumi na kisheria na dunia kwa maslahi ya
taifa."Ameongeza kusema "tunaamini umoja wetu wa kitaifa.Tunaamini
mafanikio yetu ya taifa."
Aliuchezea kamari wadhifa
Matamshi
yake hayo yalikuwa ni jibu kwa wale waliokuwa na mashaka waliosema
kwamba mafanikio hayo ya kidiplomasia ya makubaliano hayo ya nyuklia
hayawezi kutafsiriwa kwa vitendo vya faida ya kiuchumi kwa uchumi wa
nchi hiyo.
Rohani
aliuchezea kamari wadhifa wake wa urais kwa mazungumzo hayo ya nyuklia
kwa kuimarisha juhudi za kidiplomasia na zenye kuhusisha
Uingereza,China, Urusi,Ufaransa, Marekani na Ujerumani baada ya kuingia
madarakani hapo mwezi wa Augusti mwaka 2013.
Ni wiki iliopita tu amesema wananchi wa Iran wanapaswa kusubiri kwa hamu "mwaka wa neema" baada ya nchi hiyo kuondolewa vikwazo.
Saudi Arabia yakosolewa
Rouhani
pia amekosowa shutuma za Saudi Arabia kwa makubaliano hayo ya nyuklia
kwa kumtaja afisa mmoja bila ya kulintangaza jina lake ambaye alisema
kuondolewa kwa vikwazo ni hatua mbaya.
Akizungumzia
hilo amesema "siku ya utekelezaji wa makubaliano hayo tumemuona afisa
mmoja wa Saudia akielezea masikitiko yake kwamba matatizo ya kiuchumi ya
Iran yamepatiwa ufumbuzi."
Amesema
jirani hatakiwi kamwe kufanya hivyo.Muislamu hawezi kufanya
hayo.Muislamu hatakiwi katu kukasirika kwa kufarajika kwa Muislamu
mwenzake. Waislamu wote ni ndugu."
Hali ya mvutano
Kufuatia
hatua ya Saudi Arabia nchi ya ufalme wa Kisunni kutekeleza adhabu ya
kifo kwa sheikh wa Kishia Nimr al Nimr hapo Januari pili ubalozi wa
Saudi Arabia mjini Tehran ulivamiwa kitendo ambacho kililaaniwa na Rais
Rouhani.
Siku moja
kufuatia tukio hilo Saudi Arabia ilivunja uhusiano wake wa kibalozi na
Iran.Rohani amesema mlango bado uko wazi kwa diplomasia lakini hauwezi
kubakia wazi milele.
Amesema
kile wanachotaka ni kutatua mizozo ya kanda hiyo kwa kutumia busara
lakini wakati huo huo wananchi wao,serikali yao haitokubali hatua zisizo
za kidiplomasia na zisizofaa.
Utekelezaji
wa makuabaliano hayo ya nyuklia ya kihistoria kati ya Iran na mataifa
yenye nguvu yanatarajiwa kufunguwa uhalisia mpya wa kiuchumi nchini
Iran.
Zaidi ya
dola bilioni 30 za mali za Iran zilizozuiliwa nchi za nje zitaachiliwa
mara moja kwa serikali ya Iran.Jumla ya mali za Iran zilizozuiliwa nchi
za nje ni dola bilioni 100.
No comments:
Post a Comment