RAIS
Dk. John Magufuli, amesema Watanzania wote wanapaswa kuendelea
kumuombea ili aendelee na kazi yake ya kupambana na mafisadi wahujumu
uchumi na vigogo wauza dawa za kulevya nchini.
Kauli
hiyo iliitoa katika mkesha mkubwa wa kuliombea Taifa pamoja na kuuaga
mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016, uliofanyika kwenye Uwanja wa
Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais
Magufuli amesema Taifa hili kwa kipindi kirefu lilikabiliwa na vigogo
wauza dawa za kulevya, watumishi na vigogo wakwepaji wa kodi pamoja na
wizi wa dawa mahospitalini hivyo viongozi wa dini na Watanzania wote
wanapaswa kumuombea ili aweze kutumbua majipu ya mafisadi hao.
Amesema
ubadhilifu wa mali za umma umekuwa ukichangia kuzorotesha maendeleo ya
Watanzania wote kutokana na watu wachache wasiokuwa waadilifu serikalini
kuendelea na vitendo vya rushwa huku wengi wakiendelea kutaabika.
Dk.
Magufuli ambaye aliwakilishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na
Makazi, William Lukuvi, amesema kuwa viongozi wa dini wanapaswa
kuendelea kuliombea Taifa na kuwaombea watu wabaya wasiopenda maendeleo
waweze kubadilika ili nchi iweze kusonga mbele.
“Viongozi
wa dini tunapaswa kuendelea kumuombea rais wetu (Dk. John Magufuli)
aendelee kutumbua majipu haya ambayo yanasababisha maendeleo ya Taifa
letu kurudi nyuma.
“Watanzania
wenzangu tunapaswa kuendelea kuwa wamoja na kumuunga mkono Rais
Magufuli (John Magufuli) aendelee kufanya kazi yake zaidi, kuna wizi wa
dawa katika vituo vya Afya watumishi wazembe ambao hawafanyi kazi ya
umma vizuri sasa hayo yote yanahitaji ushirikiano wetu kwa rais aweze
kusimamia,” amesema Lukuvi.
Hata
hivyo katika salamu zake, aliwataka Watanzania wote kwa ujumla bila
kujali itikadi za vyama na dini zao kuendeleza umoja na mshikamano na
amani iliyopo tangu Taifa hili linapata uhuru mwaka 1964.
Hata
hivyo tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani ameweza kuwang’oa
vigogo kadhaa katika nyadhifa zao kwa tuhuma mbalimbali, kitendo ambacho
kimeonekana kuwachukiza baadhi ya viongozi na watumishi wa umma
‘mafisadi’.
Baadhi
ya viongozi waliong’olewa mpaka sasa ni aliyekuwa Mkuu wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari (TPA), Rished Bande, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah na aliyekuwa Kaimu
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Viongozi
wengine waliondolewa katika nyadhifa zao ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi
ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Diwani Msemo, aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa
Mradi wa Mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (DART), Asheria Mlambo na
aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali Reli
Tanzania (RAHCO), Benhadard Tito.
Pamoja
na kuwang’oa vigogo hao, pia baadhi ta watumishi kwenye taasisi hizo
nao wameguswa na fagio lililowaondoa katika nafasi zao, kwa sababu ya
kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili huku na wengine
wakigikishwa mahakamani.
Naye
Askofu Geoffrey Manashi, amesema Watanzania wanapaswa kuendelea
kuliombea Taifa kuendelea kuwepo amani kwani bila amani hakuna maendeleo
katika taifa lolote lile.
Amesema
uchaguzi wa mwaka 2015 watu wengi walikuwa na imani kwamba Taifa hili
litaingia katika machafuko lakini mwenyezi Mungu aliweza kulivusha
salama na kufanikiwa kumpata Rais Dk. John Magufuli, ambaye ameweza
kufanya kazi yake kwa kasi kubwa ambayo watu wengi walitarajia.
Naye
Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, Nape Nnauye amesema kuwa baadhi
ya wanasiasa na wananchi walidhani Taifa litaingia katika vurugu na
machafuko lakini wameshangaa kuona uchaguzi umemalizika kwa amani.
“Wapo
waliodhani tutaingia kwenye machafuko, lakini imeshindikana, hiyo yote
ni kutokana na Mungu wetu kutuvusha salama na tumepata rais mzuri ambaye
sasa hivi nchi nyingi zinatamani ziwe nae,” amesema Nnauye.
Naye
Askofu kutoka nchini Kongo, Debora Sanganyi, amesema Watanzania
wanapaswa kuwaombea wakongo na wao waendelee kuwa na amani iliyopo hapa
nchini kwetu.
Amesema
kuwa Kongo na wao wanatarajia kufanya uchaguzi mkuu hivyo Watanzania
wanapaswa kuwaombea na kumpata rais mchapa kazi kama Rais John Magufuli.
“Jamani
na sisi wakongo mtuombeeni kuvuka salama yale yanayokuja, tupate rais
mzuri kama wa kwenu, watanzania tuombeeni ndugu zenu,” amesema Sanganyi.
No comments:
Post a Comment