Naibu
Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia
Wambura wa pili kutoka kulia akikagua Uwanja wa Tandika ambao una
mgogoro na wapangaji wa maduka ambapo aliagiza siku saba kwa wavamizi
wote nchini kutoka kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kupisha shughuli za
michezo, wa pili kutoka kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mh.Salum
Fesal. (Picha na Benjamin Sawe-WHUSM).
Naibu
Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia
Wambura (kulia) akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Said Meck
Sadiki wakati wa ziara ya Mh. Naibu Waziri aliyoifanya katika Wilaya ya
Temeke kukagua viwanja vya wazi vilivyokusudiwa kwa ajili ya michezo
ambavyo vimemiwa na baadhi ya wananchi.
Naibu
Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia
Wambura (kulia) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Said Meck
Sadiki tayari kuanza ziara ya kukagua viwanja vya wazi vilivyokusudiwa
kwa ajili ya michezo vilivyovamiwa na baadhi ya wananchi.
Kaimu
Mkurugenzi Halmashauri ya Mainispaa ya Temeke Bw.Waziri Kombo
akimkabidhi Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mh. Anastazia Wambura taarifa ya utekelezaji kuhusiana na shughuli za
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo za Halmashauri hiyo, kulia ni Mbunge
wa jimbo la Temeke Mh.Abdalah Mtolea na kushoto ni Naibu Meya wa
Manispaa hiyo Mh.Salum Fesal.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mikono Arts aliyesimama Bw.Henry Clemensi akiongea na Naibu
Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia
Wambura kuhusu shughuli wanazofanya ili kuwasaidia wasanii wa sanaa za
uchongaji ikiwa ni pamoja na kuwatafutia soko nje ya nchi, wa kwanza
kulia waliokaa ni Mbunge wa jimbo la Temeke Mh.Abdalah Mtolea na wa
kwanza kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mh.Salum Fesal.
No comments:
Post a Comment