MWILI WA MAREHEMU ASHA BAKARI WAWASILI ZANZIBAR KWA MAZISHI LEO JANG'OMBE - LEKULE

Breaking

22 Jan 2016

MWILI WA MAREHEMU ASHA BAKARI WAWASILI ZANZIBAR KWA MAZISHI LEO JANG'OMBE

Ndege ya Shirika la Ndege la Qatar ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikiwa na Mwili wa Marehemu Asha Bakari alifariki nchini Dubai akitokea matibabuni Nchini India.Mareheme anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kianga nje kidogo ya mji wa Unguja na Maiti itasaliwa katika msikiti Mkuu wa Kwamchina saa nne asubuhi. 
Mwili wa Marehemu ukiteremshwa katika ndege kwa ajili ya maandalizi ya mazishi leo saa nne asubuhi Jangombe Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Pandu Amaer Kificho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud wakiwa uwanja wa ndege Zanzibar wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu
Ndugu na Jamaa wa Marehemu wakiwa na Viongozi wa Serikali na Chama wakisubiri kuupokea mwili wa Marehemu Uwanja wa Ndege wa Zanzibar leo jioni

Mwili wa Marehemu ukishusha katika gari baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar wakiubeba wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege Zanzibar.

No comments: