Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura, Januari 15 mjini Geneva.
Na RFI
Mazungumzo
yenye lengo la kukomesha vita nchini Syria yataanza mjini Geneva Ijumaa
hii Januari 29, msemaji wa mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini
Syria Staffan de Mistura ametangaza Alhamisi hii, ingawa makundi yote
ya upinzani bado hayajatangaza kuwa yatashiriki katika mazungumzo hayo.
"Ninathibitisha
tu kwamba mazungumzo yataanza Ijumaa", amesema Khawla Mattar, msemaji
wa Ofisi ya Staffan de Mistura kwa jibu aliloandika kupitia barua pepe.
Muda
mfupi kabla, Ofisi ya Staffan de Mistura ilitoa ujumbe wa video kwa raia
wa Syria, ambapo ilisema kuwa mazungumzo huenda yakafanyika "katika
siku zijazo."
Mwanzoni
mwa wiki hii Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Staffan de Mistura alitangaza
kwamba alituma mialiko kwa "wajumbe mbalimbali kutoka Syria"
watakaoshiriki mazungumzo hayo Ijumaa wiki hii, bila hata hivyo
kubainisha watu watakao shiriki mazungumzo hayo. Hata hivyo mpaka sasa
bado pande zote hawajaafikiana kufusu muundo wa ujumbe wa upinzani.
Kwa
upande wake Uturuki ilisema wiki hii kwamba hatoshiriki katika
mazungumzo ya amani ya Syria yatakayoanza mjini Geneva siku ya Ijumaa
kama chama cha PYD cha Wakurdi kutoka Syria hakitoshiriki, ameonya
Jumanne hii Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu.
No comments:
Post a Comment