Rais wa
zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo amekana kuwa na hatia katika
mashataka manne ya uhalifu dhidi ya ubinaadamu katika mahakama ya ICC,
miaka mitano baada ya nchi yake kukumbwa na vurugu za uchaguzi.
Gbagbo
pamoja na aliyekuwa waziri wake wa vijana Charles Ble Goude wote wawili
wameyakanusha mashtaka yanayowakabili kuhusiana na kuhusika kwao katika
machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 ambayo
yalisababisha vifo vya watu 3,000 nchini humo. Charles Ble Goude
amekanusha mashtaka dhidi yake akisema hayatambui.
Gbagbo
mwenye umri wa miaka 70 pamoja na waziri huyo wa zamani wa vijana ambaye
anadaiwa kuwa mshirika wake wa karibu wote wanakabiliwa na mashitaka
manne ya ukiukaji wa haki za binadamu yakiwemo ya mauaji na ubakaji
yanayodaiwa kufanywa na wanajeshi watiifu kwa rais huyo wa zamani
mwishoni mwa mwaka 2010 na mapema mwaka 2011 baada ya kushindwa katika
uchaguzi uliomuweka madarakani Rais Alassane Ouattara.
Bensouda akanusha uvumi kuhusu mashahidi
Awali
mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC
Fatou Bensouda alisema lengo la kesi hiyo ni kuhakikisha kuwa inafichua
ukweli kupitia njia za kisheria na kukanusha uvumi ulioonea kuwa kuna
mashahidi wa uapande wa mashitaka katika kesi hiyo waliojitoa.
No comments:
Post a Comment