Klabu ya Manchester United imeshindwa kutamba kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya kujikuta ikigaragazwa kwa bao 1-0 dhidi ya Southampton kwenye mchezo wa ligi kuu England uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford.
Ilimchukua dakika saba na sekunde 43 tu, Charlie Austin kuiandikia bao Southampton akitokea benchi dakika ya 79 kuchukua nafasi ya Mane. Austin aliweka mpira wavuni dakika ya 87 akiunganisha kwa kichwa krosi ya James Ward-Prowse na kuipa ushindi timu yake ikiwa kwenye uwanja wa ugenini.
Kipigo cha leo kinaifanya Man United kuendelea kubaki nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi, ikiwa na point 37 katika michezo 23. Huo ni mchezo 6 kwa Man United kupoteza toka kuanza kwa msimu wa 2015/2016.
Vikosi vya timu zote vilivyocheza mchezo wa leo Manchester United vs Southampton
Takwimu za mchezo kati ya Manchester United vs Southampton
Matokeo ya mechi nyingine za EPL zilizopigwa leo Jumamosi January 23
Norwich 4-5 Liverpool
Crystal Palace 1-3 Tottenham
Leicester City 3-0 Stoke City
Man Utd 0-1 Southampton
Sunderland 1-1 Bournemouth
Watford 2-1 Newcastle Utd
West Brom 0-0 Aston Villa
No comments:
Post a Comment