WAZIRI
wa Katiba na Sheria,Dk.Harrison Mwakyembe amesema kuwa suala la
kuanzisha mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi wanafanyia kazi na
muda sio mrefu watatoa taarifa juu ya hatua walizofikia.
Dk.Mwakyembe
ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Ofisi ya Mkurugenzi wa
Mashitaka nchini (DPP),amesema kuwa suala mahakama linafanyiwa kazi kwa
karibu na ofisi yake kutokana na ahadi ya Rais Dk.John Pombe Magufuli
wakati wa kampeni.
Mwakyembe
amesema kuwa watu ambao wanaweza kuleta maendeleo ya nchi ni vyombo
vilivyo katika maamuzi ya kisheria hivyo lazima viweze kufanya kazi kwa
wananchi kwa kutenda haki.
Amesema
kuwa baadhi ya watendaji wa taaluma ya sheria sio waaminifu kwa
kujihusisha na rushwa na kufanya watendaji wote kuharibika kwa sababu ya
mtu mmoja.
Mwakyembe
amesema yeye ni mwanasheria na kuongeza kuwa kuna’ majipu’katika tasnia
ya taaluma ya sheria na kuwataka majipu hayo yatumbuliwe kabla ya Rais
Dk.John Pombe Magufuli hajayatumbua bila sindano ya kupunguza maumivu
(Ganzi).
Mwakyembe
amesema kuwa wanajua changamoto ya mawakili wa serikali wanazokumbana
nazo ikiwemo miundombinu pamoja na mfumo wa maisha wanayoishi hivyo
serikali itafanya uwezeshaji kadri ya uwezo wao.
Mkurugenzi
wa Mashitaka nchini,Buswello Mganga amesema katika mafanikio
walioyapata ni pamoja kushinda kesi nane za dawa za kulevya kwa
watuhumiwa kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 hadi 30.
No comments:
Post a Comment