MAHAKAMA
Kuu Kanda ya Dodoma imefutilia mbali kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na
mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jonathan Njau kupinga ushindi wa
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (CHADEMA).
Katika madai yake ya msingi, Njau alikuwa akipinga matokeo na kutaka kura kuhesabiwa upya.
Shauri
hilo lilikuwa mbele ya Jaji Berkel Sehel ambapo mgombea wa ubunge
kupitia chama cha Mapinduzi CCM Jonathan Njau alishindwa kwenye uchaguzi
kwenye jimbo hilo mwaka 2010 na 2015.
Njau Aliwasilisha ombi mahakamani la kutaka kesi hiyo kufutwa kwani hana haja ya kuendelea na shauri hilo.
Awali
mlalamikaji aliwahi kupeleka mahakamani mara mbili maombi ya ombi la
kusamehewa kwa gharama za kesi kiasi cha milioni 15 lakini maombi hayo
yalitupwa
Lisu amesema Mahakama kuu ilishatamka mwaka 2010 kuwa kesi za uchaguzi si za kuendea kwa papara bila umakini wowote.
No comments:
Post a Comment