Aliyekuwa
mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Edward Lowassa, amemtembelea Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye,
katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Hosptitali ya Taifa
Muhimbili alikolazwa.
Lowassa
ambaye alifika hospitalini hapo jana saa 7:00 mchana akiwa na mke wake
Regina, aliwapongeza viongozi wengine ambao wamekwisha kufika
hospitalini hapo kumjulia hali Sumaye, wakiwamo Rais John Magufuli, Rais
Mstaafu na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa.
Lowassa alisema hilo ni jambo jema la kiungwana, la kuheshimiana na kutendeana mema.
Wengine
waliomtembelea Sumaye hospitalini hapo ni Waziri Mkuu Mstaafu, Dk.
Salim Ahmed Salim na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Prof. Mwesiga
Baregu.
Lowassa na mkewe walifika hospitalini hapo muda mfupi baada ya Prof. Baregu na Dk. Salim kumuona Sumaye.
Akizungumza baada ya kutembelewa na hospitalini hapo, Sumaye alisema anaendelea vizuri.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi, alisema hali ya mgonjwa huyo imeendelea kuimarika kila siku.
Sumaye alilazwa katika taasisi hiyo siku sita zilizopita kwa matibabu ya moyo.
No comments:
Post a Comment