Linex kulamba shavu Sweden - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Tuesday, 5 January 2016

Linex kulamba shavu SwedenLinex 
Mkali wa Bongo Fleva Sunday Mjeda ‘Linex’.
DEOGRATIUS MONGELA

MSANII wa Muziki wa RnB, Mtanzania mwenye maskani yake nchini Sweden, Khairat Carlo Omar, ’Dati’ amemshirikisha kwenye songi lake Mkali wa Bongo Fleva Sunday Mjeda ‘Linex’ na kumtumia tiketi ya ndege kwa ajili ya kufanya video nchini humo.

Dati anayetamba na wimbo wake wa Can Do uliotengenezwa na Prodyuza Fundi Samweli na video ikiwa imeshutiwa na wakali kama Hanscana na Khalfan, ameweka mipango ya kufanya wimbo mpya na Linex ambapo alisema kuwa wimbo huo ni ladha mpya kabisa kusikika Bongo.

“Mipango yote inaenda sawa na wimbo wangu na Linex utakuwa ni wa Kiswahili, lengo la kufanya video huku Sweden ni kuutanua muziki wangu na kukitangaza Kiswahili, hii ni kwa wale mashabiki wa Linex,” alisema Dati.
Post a Comment