Joe Allen amefanya Arsenal washindwe kuondoka na point tatu Anfield, cheki ilivyokuwa (+Pichaz&Video) - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Thursday, 14 January 2016

Joe Allen amefanya Arsenal washindwe kuondoka na point tatu Anfield, cheki ilivyokuwa (+Pichaz&Video)Mechi za Ligi Kuu Uingereza zimeendelea kama kawaida kwa kupigwa michezo saba usiku wa January 13, miongoni mwa michezo iliyochezwa usiku wa January 13 ni mchezo kati ya Liverpool ambao waliwakaribisha Arsenal katika dimba la Anfield.
3024E18E00000578-3398223-image-a-72_1452723685027
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Anfield lenye mashabiki ambao wagumu kukata tamaa ya kuacha kushangilia hata kama timu imefungwa, ulimalizika kwa Arsenal na Liverpool kufungana kwa sare ya magoli 3-3. Mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili, kwani timu zote mbili zilikuwa zikihangaika kusaka point tatu.
30242B3900000578-3398223-image-a-5_1452719468407
Liverpool ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la mapema, kwani dakika ya 10 Roberto Firmino alifanikiwa kupachika goli la kwanza, goli ambalo  Aaron Ramsey alisawazisha dakika nne baadae, Roberto Firmino alirudi tena nyavuni dakika ya 19 baada ya kupachika goli la pili. Arsenal walianza kuja juu kupitia kwa mshambuliaji wao wa kimataifa wa Ufaransa Oliver Giroud walifanikiwa kufunga goli mbili dakika ya 25 na 55 kipindi cha pili, Arsenal wakiwa na imani ya kuondoka na point tatu Joe Allen aliisawazishia goli Liverpool dakika ya 90 ya mchezo.
Matokeo ya mechi nyingine za Uingereza January 13
  • Chelsea 2 – 2 West Bromwich Albion
  • Manchester City 0 – 0 Everton
  • Southampton 2 – 0 Watford
  •  Stoke City 3 – 1 Norwich City
  • Swansea City 2 – 4 Sunderland
  • Tottenham Hotspur 0 – 1 Leicester City
302420CA00000578-3398223-Liverpool_striker_Roberto_Firmino_centre_rifles_his_side_into_th-a-84_1452724033137
Video ya magoli ya Liverpool Vs ArsenalPost a Comment