Esther Bulaya Ashinda Kesi Ya Kupinga Ushindi Wake Iliyofunguliwa na Stephen Wassira - LEKULE

Breaking

25 Jan 2016

Esther Bulaya Ashinda Kesi Ya Kupinga Ushindi Wake Iliyofunguliwa na Stephen Wassira


Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na wapambe  wa  aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Bunda Mjini kwa tiketi ya CCM, Stephen Wassira kwa madai kuwa waleta maombi hawakuwa na haki kisheria ya kufungua kesi hiyo

Wapambe  wa  Wassira walifungua kesi Mahakama kuu  kupingamatokeo ya uchaguzi huo wakidai kuwa uligubikwa na udanganyifu na hujuma dhidi ya mgombea wao ( Stephen Wassira ) ikiwa ni pamoja na kutofautiana kwa idadi ya wapiga kura kwenye kituo na jumla ya kura zilizoonekana kwenye fomu za matokeo. Wapambe hao waliiomba mahakama kubatilisha ushindi wa Bulaya.

Bulaya alihamia Chadema akitokea CCM na kupewa nafasi ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita na hatimaye kumshinda Stephen  Wassira aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka mingi na waziri wa serikali ya awamu ya nne.

==>Kupitia Facebook, Esther Bulaya ameandika kuhusu hukumu ya kesi hiyo:

"Nilimshinda Wasira kwa wananchi, na leo nimemshinda kisheria, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya Uchaguzi dhidi yangu, iliyofunguliwa na wapambe wa wasira. 
 
"Mungu husimama na watu waliowema. Nakutumaini mungu wangu na wewe ndiye mlinzi wangu.Asante sana Wananchi wangu wa Bunda Mjini mliokwenda Mwanza kusikiliza Hukumu. 
 
"Mbunge wenu nipo dodoma tayari kwa kuanza vikao vya Bunge Kesho."



No comments: