Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala jana alimtembelea na kumjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Kadinali Polycarp Pengo aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Akiongelea
kuhusu hali ya Kadinali Pengo, Mhe. Kigwangala alisema kuwa Kadinali
Pengo yuko salama katika mikono ya madaktari wa taasisi hiyo na hali
yake inaendelea vizuri ambapo ameweza kuongea nae ana kwa ana kiasi cha
kuweza kukaa na kuongea.
‘’Mwanzoni
alilazwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo hapa jijini Dar es Salaam,
lakini ikaonekana ni vema akiletwa hapa kwenye Hospitali yetu hii ya juu
kabisa ya matibabu ya moyo (Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete), hivyo
napenda kuwapa taarifa Watanzania kwamba yuko salama kabisa katika
mikono ya madaktari wetu na hali yake inaendelea vizuri.’’
Awali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli
akiongozana na Mkewe mama Janeth Magufuli walienda pia kumjulia hali
Kadinali Pengo katika taasisi hiyo na kumtakia afya njema ili aweze
kuendelea na shughuli zake za kiroho.
Kadinali
Pengo alifikishwa katika taasisi hiyo ya moyo kwa ajili ya kuchunguzwa
afya yake ambapo afya yake kwa sasa imezidi kuimarika.
Hapa kuna video nzima ya Dr. Kigwangala akimjulia hali
No comments:
Post a Comment