Wakati
watu mbalimbali wakimminia sifa Rais John Magufuli kwa kubana matumizi,
aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga amesema
uwingi wa makatibu wakuu unakinzana na dhana ya yake ya kupunguza ukubwa
wa Baraza la Mawaziri.
Dk
Mahanga alikuwa Naibu Waziri wa Lazi na Ajira tangu mwaka 2008 na
hakuwahi kuhamishwa wala kupandishwa hadi ngazi ya uwaziri hadi Serikali
ya Rais Jakaya Kikwete ilipomaliza muda wake na baadaye kujiunga na
Chadema.
Katika
waraka wake alioutoa kwenye mitandao ya kijamii, Dk Mahanga alimkosoa
Rais Magufuli akisema ameongeza ukubwa wa Baraza la Mawaziri baada ya
kuteua makatibu wakuu 27 wakati anawaaminisha wananchi kwamba wizara ni
15 tu.
Dk
Magufuli ameunda baraza lenye mawaziri 15, na manaibu waziri 19 na
hivyo kufanya baraza lake kuwa na jumla ya mawaziri 34, tofauti na
baraza lililopita lililokuwa na mawaziri 55.
Uamuzi
wa kupunguza idadi ya wizara ulikumbana na changamoto ya nafasi za
makatibu, ambao hata hivyo baadhi amewarudisha wizarani ambako
watapangiwa kazi na kubakiwa na makatibu 27.
“Si
kweli kwamba kapunguza ukubwa wa Serikali, bali kaongeza ukubwa wake.
Sina hakika kama wasaidizi wa Rais wamemshauri na kumweleza kwamba
wizara si ofisi ya waziri bali wizara ni ofisi ya katibu mkuu,” alisema Dk Mahanga akifafanua kuwa katibu mkuu ndiye mtendaji mkuu wa wizara na afisa masuhuli.
Alisema
katibu mkuu ndiye mwenye dhamana ya utendaji na ndiyo maana hata katika
ngazi ya kata, ofisi inaitwa ofisi ya ofisa mtendaji wa kata na si
ofisi ya diwani.
Kwa
maana hiyo, Dk Mahanga, ambaye kitaaluma ni mhasibu, alisema Rais
alipounda Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ambazo awali zilikuwa mbili
tofauti na kuteua makatibu wakuu watatu, kiuhalisia hakuunganisha
wizara mbili kuwa moja bali ameunda wizara tatu kutoka mbili za awali.
“Ongezeko
la gharama kwa kuongeza waziri mmoja ni ndogo sana kulinganisha na
kuongeza katibu mkuu mmoja. Waziri anapoteuliwa tayari anakuwa ni mbunge
mwenye mshahara wake wa ubunge na kinachoongezeka ni kama laki tano tu
juu ya ule mshahara wa ubunge na gharama nyingine ndogo za gari, pia
mishahara na gharama za katibu muhtasi, msaidizi na dereva,” alisema Dk Mahanga.
Alisema
kwa ujumla ahadi ya Rais Magufuli aliyotoa kwenye kampeni kwamba
ataunda Serikali ndogo, hakuitimiza badala yake ameongeza ukubwa wa
Serikali.
Wakati
wa kampeni na alipoapishwa, Rais Magufuli alisema ataunda baraza dogo
la mawaziri, hiyo ilijenga shauku kwa wananchi kufahamu kiwango cha
ukubwa au udogo wa baraza hilo ikilinganishwa na mabaraza yaliyoundwa na
watangulizi wake, tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.
Dk Magufuli pia alitoa ahadi hiyo alipozindua Bunge Novemba mwaka jana mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment