CCM Yaomba Radhi Kutokana na Maneno ya Kibaguzi Kwenye Bango Katika Sherehe za Mapinduzi - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Tuesday, 12 January 2016

CCM Yaomba Radhi Kutokana na Maneno ya Kibaguzi Kwenye Bango Katika Sherehe za Mapinduzi

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na mmoja wa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi.

Ujumbe huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na Mshikamano wa Kitaifa.

Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
12/01/2016
Post a Comment