Al-Shabab wako 'huru' kushiriki soka Somalia - LEKULE

Breaking

11 Jan 2016

Al-Shabab wako 'huru' kushiriki soka Somalia

Wapiganaji wa Alshabaab
Mkuu wa shirikisho la soka nchini Somalia amesema kuwa kundi la wapiganaji wa al-Shabab liko huru kushiriki katika ligi kuu ya soka nchini humo.
Abdiqani Said Arab amemuambiwa mwandishi wa BBC jijini Nairobi John Nene kwamba iwapo wapiganaji hao wanataka kushiriki watepewa fursa.
''Hatuwapingi na hawatupingi," alisema.
Kundi la al-Shabab linaloendesha itikadi kali, limewaagiza wanasoka kuvaa suruali ndefu na limepiga marufuku muziki katika maeneo linalodhibiti.
Hata hivyo, Bw Arab amesema kuwa anaamini kwamba wafuasi wa kundi hilo wanahudhuria mechi za soka lakini akakataa kutoa maelezo zaidi.
Soka Somalia
Mwezi Uliopita,mechi moja nchini Somalia ilipeperushwa moja kwa moja katika runinga ya kitaifa kwa mara ya kwanza.
''Ligi hiyo inawavutia wachezaji wa kigeni kutokana na hali shwari ya usalama'',alisema Bw Arab.
''Zaidi ya wachezaji 20 wa kigeni wanashiriki katika ligi yetu," katika vilabu 6, aliongezea.
Vikosi vya Umoja wa Afrika vinavyoungwa mkono na serikali vimeimarisha udhibiti wao wa maeneo mengi yaliokuwa yakidhibitiwa na kundi hilo ambalo linapigana kuweka utawala wa kiislamu.

No comments: