WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA AFUNGUA KITUO CHA UTAMADUNI WA CHINA NCHINI TANZANIA - LEKULE

Breaking

1 Dec 2015

WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA AFUNGUA KITUO CHA UTAMADUNI WA CHINA NCHINI TANZANIA

Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (kushoto) akifungua kituo cha utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mkurugenzi wa Utamaduni toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko.
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) akipata maelekezo toka kwa Mshauri wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. GAO Wei (kulia) wakati Waziri Mkuu akifungua kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Baadhi ya wanafunzi wa Kitanzania wanaojifunza lugha ya Kichina katika kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania wakiimba nyimbo kwa lugha ya Kichina mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kituo hicho.
Kundi la Muziki la Zinijncheng kutoka chuo Kikuu cha Sanaa ya Muziki cha China kikitoa burudani kwa mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania.

Mshauri wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. GAO Wei akitoa ufafanuzi wa picha za matukio mbalimbali kwa Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) mara baada ya Waziri Mkuu Mstaafu kufungua kituo cha utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo. 

No comments: