WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema hana orodha ya
majina ya watu wanaouza dawa za kulevya na hana muda wa kushughulika na
hiyo inayoitwa orodha.
Badala yake, amesema chini ya uongozi wake ataweka mifumo itakayosaidia kudhibiti uingizaji wa dawa hizo nchini.
Akizungumza
jana na waandishi wa habari Dar es Salaam baada ya kufanya kikao na
maofisa wa ngazi ya juu wa Polisi, Kitwanga alisema wamekubaliana
kuhakikisha dawa za kuleya zilizoko nchini zinakamatwa na kuteketezwa.
“Mimi
hapa nilipo sina orodha ya wauza dawa za kulevya na wala Rais
hajanipatia hiyo orodha na siamini kama Rais anayo...ila ninachowaambia
ni kwamba tumekubaliana kuweka mifumo mizuri ya kuwakamata watu wote
ambao watakutwa na dawa hizo,” alisema Kitwanga.
Alisema mifumo hiyo haitajali ukubwa na nafasi ya mtu kwenye jamii.
“Maana mifumo hii tunayoiweka haijali vigogo wala sisimizi na
nawahakikishia kwamba tumejipanga kumaliza tatizo hili la dawa za
kuleya,” alisema.
Alisema
katika kikao hicho wamekubaliana kuongeza nguvu kuhakikisha
wanawakamata watu wote ambao wanahusika na biashara haramu ya kuingiza
dawa za kulevya na kuzisambaza nchini.
Akizungumza
kutokuwepo kwa polisi katika Bandari ya Dar es Salaam, alisema
wanaendelea kufanya mazungumzo na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA)
kuona utaratibu mzuri wa kupeleka ulinzi kwenye eneo hilo ili kuweza kudhibiti utoroshaji wa vitu mbalimbali ambavyo vinatoka bila utaratibu.
Katika hatua nyingine, Kitwanga aliwataka polisi kuwashitaki watu kwa kesi walizo nazo na sio kuwabambika kesi watu wasio na hatia na kusababisha kufungwa kwa kesi zisizowahusu.
Katika hatua nyingine, Kitwanga aliwataka polisi kuwashitaki watu kwa kesi walizo nazo na sio kuwabambika kesi watu wasio na hatia na kusababisha kufungwa kwa kesi zisizowahusu.
No comments:
Post a Comment