WATU wawili wakiwemo Mwanasheria na Mwalimu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama za kumuua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva na familia yake.
Washitakiwa
hao, Mwalimu Samwel Gikaro (30) na Mwanasheria Angela Mbonde (32)
walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu
Mkazi Thomas Simba.
Wakili
wa Serikali, Hellen Moshi alidai kati ya Oktoba 23 na Novemba 16, mwaka
huu katika maeneo tofauti Dar es Salaam na maeneo mengine nchini,
washitakiwa na wengine ambao hawajafika mahakamani, walikula njama za
kumuua Jaji Lubuva na familia yake.
Washitakiwa
walikana mashitaka na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi
hiyo unaendelea na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Wakili wa upande wa utetezi, Moses Kaluwa ambaye alifika mahakamani hapo kwa niaba ya Wakili Peter Kibatala, aliiomba mahakama itoe dhamana kwa washitakiwa kwa kuwa mashitaka yanayowakabili yana dhamana.
Wakili wa upande wa utetezi, Moses Kaluwa ambaye alifika mahakamani hapo kwa niaba ya Wakili Peter Kibatala, aliiomba mahakama itoe dhamana kwa washitakiwa kwa kuwa mashitaka yanayowakabili yana dhamana.
Wakili
Moshi alidai Jamhuri inatambua mashitaka hayo yana dhamana kisheria,
lakini inaomba dhamana izuiliwe kwa muda hadi watakapoona inafaa kwa
sababu ya asili ya kosa, washitakiwa hawawezi kuwa nje wakati upelelezi
unaendelea.
Hata
hivyo, Wakili Kaluwa alidai sababu zilizotolewa na upande wa jamhuri
hazina msingi kisheria, suala la msingi ni mashitaka yanayowakabili kuwa
na dhamana na washitakiwa wapo tayari kutimiza masharti yatakayotolewa
na mahakama.
Hakimu
Simba alisema pamoja na mashitaka hayo kuwa na dhamana kisheria,
kutokana na kosa pamoja na hatua ya upelelezi, mahakama imekubali hoja
za upande wa jamhuri hivyo washitakiwa watakuwa rumande. Kesi itatajwa
tena Desemba 15, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment