Mkurugenzi
wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo (wa nne kushoto)
akisisitiza jambo katika kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wakuu
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na Business Times. Menejimenti ya PSPF ipo
katika ziara ya kutembelea vyombo vya habari kwa lengo la kutolea
ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali ya Mfuko na kutambulisha huduma mpya
ya Bima ya Afya. (Picha zote na Abdul Njaidi).
Mkurugenzi
Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Wahariri wa Kampuni
ya Mwananchi Communications Limited (MCL) alipotembelea Makao Makuu ya
MCL, Tabata Relini jijini Dar es salaam, kulia ni watendaji wa PSPF.
Meneja
Mkuu wa Business Times Limited Bw. Aga Mbuguni (kushoto) akipokea
machapisho mbalimbali ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF kutoka kwa Mkurugenzi
mkuu wa Mfuko huo Bw. Adam Mayingu baada kikao cha watendaji wakuu wa
taasisi hizo kilichofanyika Makao Makuu ya Business Times jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Bw. Francis Nanai
(kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugezi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni
wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, baada ya kikao kazi kati ya Wahariri wa
Mwananchi na Watendaji wa PSPF, kushoto ni Bw. Daniel Mwaijega Meneja
Utawala Idara ya Habari na kulia ni Bibi. Matlida Nyalu Afisa wa Mpango
wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF.
MKURUGENZI
Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu aliongoza ujumbe wa watendaji wakuu wa
PSPF kutembelea vyumba vya habari vya magazeti ya Mwananchi na Majira,
ikiwa ni utaratibu wa PSPF wa kutembelea vyombo vya habari kwa lengo la
kufahamiana, kutolea ufafanuzi masuala mbalimbali na kupokea ushauri wa
kuboresha huduma za PSPF.
Katika
ziara hiyo iliyofanyika Desemba 2, 2015, Mkurugenzi wa PSPF aliongozana
na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabrilel Silayo, Mkurugenzi
wa Uendeshaji, Bibi Neema Muro, Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Andrew
Mkangaa, Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi, Bibi. Costantina
Martin, Afisa kutoka Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Bibi.
Mathilda Nyallu na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi.
Kituo
cha kwanza cha safari hiyo ilikuwa katika ofisi za gazeti la Majira
wachapishaji wa Gazeti la Majira na Business Times ambapo walikutana na
watendaji wakuu wa kampuni hiyo.
Pia
viongozi hao wa PSPF walitembelea ofisi za Mwananchi Communications
zilizopo Tabata, ambapo walikutana na watendaji wakuu wa gazeti hilo.
Katika maeneo yote watendaji wa PSPF walijibu maswali mbalimbali,
walipokea ushauri na kutambulisha huduma ya Bima ya Afya inayotolewa na
PSPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
“Lengo
la ziara hizo ni kuwatembelea wenzetu wa vyombo vya habari kwa lengo la
kufahamiana, kutolea ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali ya PSPF na
kujifunza kutoka kwao jinsi ya kuboresha huduma zetu, pia kwa sasa
tunatangaza huduma yetu mpya ya Bima ya Afya,hivyo tupo katika mpango wa
kuwaelimisha waandishi wa habari ili na wao waweze kuelimisha umma juu
ya mpango huo ambao ni mkombozi kwa watanzania wengi…huu ni mwendelezo
kwani tulianza ziara hizi tangu mwaka jana,” alifafanua Bw. Mayingu.
No comments:
Post a Comment