Katibu mkuu wa chama cha ADA-TADEA, John Shibuda akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na viongozi wa mashirkiano ya umoja wa
vyama vya UDA, TADEA,UDP,UPDP,na SAU kwa kuwaomba viongozi wa
ZEC,CUF,CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili waweze kukutana na
kuzungumza pamoja kuhusiana na migoro wa kisiasa nchini humo, ameyasema
leo jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu wa chama cha ADA-TADEA, John Shibuda katikati
akizungumza na waandishi a habari jijini Dar es Salaam leo, kutoka
kushoto ni Makamu Mwenyekiti SAU na mjumbe wa URAWU, Yusuf Manyanga, na
Mwenyekiti wa Taifa UPDP, Katibu mkuu wa URUWA, Comrade Fahami Dovutwa
na kulia ni Naibu Katibu mkuu wa UDP na mjumbe wa URAWU, Izaak Cheyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimksikiliza Katibu mkuu wa
chama cha ADA-TADEA, John Shibuda wakati akizungumza leo katika mkutano
uliofanyika katika hoteli ya Legho jijini Dar es Salaam.
UMOJA wa Rufaa ya Wananchi (
URUWA
)
unaoundwa na viongozi wa Mashirikiano ya umoja wa vyama vya
UDA,TADEA,UDP,UPDP na SAU (URUWA) wameomba kukutana na viongozi wa ZAC,
CUF,CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa chama cha ADA-TADEA, John Shibuda wakati akizungumza na waandishi wa habari
katika Hoteli ya Legho
jijini Dar es Salaam leo.
Ombi hilo limekuja baada ya viongozi hao kutaka kuelimishwa kuhusu sintofahamu ya uchaguzi wa Zanzibar
na kuwataka viongozi wa zanzibar waache kutoa kauli na matamko ya mivuno iliyo na tija kwa wanchini humo.
Pia Shibuda amesema kuwa wanataka ifahamike kwamba ugomvi wa Akili
makini na giza totoro ni mwanga nao wameamua kuwa mwanga na kubaini
kilichomo katika hili giza la mabishano kati ya
ZAC, CUF,CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wakati huhohuo Shibuda amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, John Pombe Joseph Magufuri pamoja na wasaidizi wake wakuu
Makamu wa Rais, Samia Suluhu pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa
kuwaunga mkono kwa juhudi zao za utumishi, uaminifu na utiifu kwa ustawi
wa maendeleo ya jamii na Taifa.
No comments:
Post a Comment