Rais wa Ujerumani Joachim Gauck akikagua gwaride la heshima,Jordan
Viongozi
wa ngazi ya juu wa Ujerumani wako katika ziara tofauti wakilenga
kufanikisha juhudi za kuleta amani na maridhiano katika nchi kadhaa
zinazokabiliwa na migogoro,kuanzia Afghanistan,hadi mashariki ya Kati.
Rais
Joachim Gauck yuko Jordan alikowasili akitokea Israel na Palestina
ambako amezitolea mwito pande zote mbili kutoa nafasi ya pili kwa
mazungumzo ya kusaka amani katika eneo hilo.
Tukianzia
na ziara ya rais Joachim Gauck mashariki ya kati ambapo leo amezungumza
na mfalme Abdullah wa Jordan amebaini kwamba Ujerumani inaunga mkono
mapambano ya kukabiliana na kundi la wanamgambo wa itikadi kali
linalovuruga usalama katika nchi za Syria na Iraq pamoja na kuwasaidia
wakimbizi wanaotoroka mgogoro katika nchi ya Syria.
Aidha
rais huyo wa Ujerumani ameisifu Jordan kwa kuwa mshirika mkubwa
anayesaidia katika kulishughulikia wimbi la wakimbizi kutoka Syria.
Jumapili
rais huyo wa Ujerumani alipokuwa ziarani Jerusalem aliwatolea mwito
viongozi wa Palestina na Israel kuweka pembeni mivutano na kukaa tena
katika meza ya majadiliano kutofuta makubaliano ya amani.
Steinmeier Iraq
Ama
kwa upande mwingine Juhudi za kutuliza migogoro zinafanywa pia na
waziri wa mambo ya nje Frank Waltersteinmeier aliyeko Iraq ambako hii
leo amekutana na waziri mkuu Haider al Abadi ambaye ameitaka Ujerumani
kutoa msaada zaidi katika mapambano na kundi la dola la kiislamu nchini
Iraq.
Iraq
imeitaka serikali ya Ujerumani kusaidia katika kutoa mafunzo kwa vikosi
vyake katika wakati ambapo wanajeshi wa Ujerumani wanatoa mafunzo kwa
wanajeshi wakikurdi tu kaskazini mwa Iraq.Aidha waziri Steinmeir kwa
upande wake ametumia nafasi ya ziara hii kuzungumzia hatua ya hivi
karibuni ya jeshi la Iraq kufanikiwa kuidhibiti tena miji kadhaa ya Iraq
ambayo awali ilidhibitiwa na dola la Kiislamu.Ziara ya Steinmeier ni ya
ghafla nchini Iraq iliyoanza hapo jana.
Von Der Leyen Afghanistan
Halikadhalika
waziri wa ulinzi Ursula von Der Leyen naye yupo nchini Afghanistan
tangu jana ambako aliwatembelea wanajeshi wa Ujerumani huko Kaskazini
mwa nchi hiyo ikiwa ni ziara inayofanyika baada ya serikali ya Ujerumani
hivi karibuni kutoa uamuzi wa kutanua hatua za kupeleka wanajeshi wake
nchini humo.Katika ujumbe wake nchini humo Von Der Leyen amewaambia
waafghanistan kwamba wanajeshi wa Ujerumani wataendelea kubakia
Afghanistan.Wanajeshi wa Ujerumani wako Mazar-I-Sharif ambako wanajeshi
1500 kutoka nchi 21 za Jumuiya ya Nato wamepiga kambi wengi wakiwa ni
kutoka Ujerumani.Ujerumani inapanga kuongeza wanajeshi wake huko kutoka
850 hadi 980.
Mwandishi Saumu Mwasimba
Mhariri:Abdul-Rahman
No comments:
Post a Comment