UEFA YATANGAZA KIKOSI BORA LIGI YA MABINGWA - LEKULE

Breaking

17 Dec 2015

UEFA YATANGAZA KIKOSI BORA LIGI YA MABINGWA

UEFA imetangaza Kikosi Bora cha Wachezaji Bora waliotamba Hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu huu.
Kikosi hicho kimetangazwa mara baada ya kufanyika Droo ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Kikosi hicho kinaongozwa na Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo, akishirikiana na Mafowadi Hulk na Thomas Muller huku Ligi Kuu England ikitoa Wachezaji wawili, Willian wa Chelsea na Raheem Sterling wa Man City.

Lakini, wakati Mabingwa Watetezi wa UEFA CHAMPIONS LIGI, FC Barcelona, wakiwa hawana hata Mchezaji mmoja katika hiyo 11 Bora ya Klabu Ulaya, Bayern Munich na Paris Saint-Germain, zinatamba zikiwa na Wachezaji Wawili wawili kwa kila Klabu.

TIMU KAMILI:
-Mfumo 4-3-3
KIPA: Kevin Trapp (Paris Saint-Germain)

-Licha ya kukabiliwa na mashambulizi makali katika Kundi ambalo walikuwa na Real Madrid na Shakhtar Donetsk, PSG walifungwa Bao 1 tu katika Mechi 6 za Kundi lao huku Kipa kutoka Germany Trapp akitamba. 


FULBEKI KULIA: Andrea Barzagli (Juventus)
-Akiwa Uwanjani na Juventus, Mchezaji huyu aliewahi kutwaa Kombe la Dunia na Italy, walifungwa Bao 1 tu na yeye ndie aliemtengenezea Alvaro Morata Bao walipoifunga Sevilla. 


SENTAHAFU: Thiago Silva (Paris Saint-Germain)
-Licha ya kutemwa na Brazil hivi sasa, Silva ni nguzo imara kwa PSG na kuisaidia kufuzu. 


SENTAHAFU: Diego Godin (Atletico Madrid)
-Ni Sentahafu ambae alisimama imara kwa Timu yake kuruhusu Bao 3 tu hatua ya Makundi. 


FULBEKI KUSHOTO: David Alaba (Bayern Munich)
-Alicheza Mechi 4 tu za Kundi lao na kusaidia kupata ushindi wa kishindo katika Mechi 3 moja ikiwa dhidi ya Arsenal huku yeye akifunga Bao 1 na kutengeneza 1.


KIUNGO KULIA: Sven Kums (Gent)
-Kwa kufunga Bao 1 na kutengeneza 2, Kums amestahili kuwemo Kikosini. 


KIUNGO KATI: Willian (Chelsea)
-Mbrazil huyu alipiga Bao 4 za Frikiki murua na kuisaidia Chelsea kufuzu. 


KIUNGO KUSHOTO: Raheem Sterling (Manchester City) 
-Aliifungia City Bao 3 na kutengeneza 1. 


FOWADI KULIA: Thomas Muller (Bayern Munich)
-Alifunga Bao 5 hatua za Makundi. 


SENTAFOWADI: Hulk (Zenit St Petersburg)
-Bao 3 na kutengeneza Bao 3 kumempa nafasi Kikosini. 


FOWADI KUSHOTO: Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
-Ameweka Rekodi ya kupiga Bao 11 hatua ya Makundi ikiwemo Hetitriki dhidi ya Shakhtar Donetsk na Bao 4 walipocheza na Malmo.

No comments: