Mkurugenzi
wa Undelezaji wa Mafuta na Gesi Asilia Dk. Wellngton Hudson (kushoto),
akitoa mfano wa Hundi ya shilingi 15,000,000, kwa uongozi wa Mkoa wa
Mtwara na Klabu ya Mpira wa Miguu ya Ndanda, kuanzia kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, Mkurugenzi wa Klabu ya Ndanda
Athuman Kambi na Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Alfred Cosmas Luanda.
Mkurugenzi
wa Undelezaji wa Mafuta na Gesi Asilia Dk. Wellngton Hudson (pili
kushoto), akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi 10,000,000 kwa uongozi
wa Wilaya ya Mtwara kwa ajili ya kumalizia jengo la Ofisi ya Kata ya
Ufukoni, Uongozi wa Wilaya ya Mtwara uliwakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara, Fatuma Ali (wa tatu kulia), Meneja Mawasiliano-TPDC Marie
Msellemu (wa kwanza kushoto).
SHIRIKA
la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kwa kutambua dhana ya
uwabikaji kwa jamii (Social Corporate Responsibility) mwishoni mwa wiki
limekabidhi msaada kwa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Ndanda na kata ya
Ufukoni Mkoani Mtwara. TPDC imefikia hatua hii baada ya kupokea maombi
ya uhitaji kutoka kwa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Ndanda na Kata ya
Ufukoni Mkoani Mtwara.
Klabu
Mpira wa Miguu ya Ndanda imenufaika na kiasi cha Shilingi milioni
15,000,000 kwa ajili ya kuiwezesha kushiriki vyema na kuleta ushindani
katika Ligi Kuu ya Mpira wa Miguu Tanzania Bara.
Aidha,
TPDC imechangia kiasi cha shilingi milioni 10,000,000 kwa ajili ya
kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Ufukoni. Hatua hii imekuja ikiwa
jitihada za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.
Dk. John Pombe Mangufuli kuhakikisha utawala bora unatekelezwa kwa
vitendo.
Hata
hivyo, Mkurugenzi wa Undelezaji wa Mafuta na Gesi Asilia Dk. Wellngton
Hudson alisema TPDC itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika
kusukuma gurudumu la maendeleo katika maeneo yaliyo jirani na
miundombinu ya Mradi wa gesi asilia pale linapokuawa na uwezo wa
kifedha.
No comments:
Post a Comment