Meneja
Mkuu wa Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC),
Mhandisi Boniface Njombe akichangia mada wakati wa Warsha ya siku mbili
inayofanyika Jijini Dar es Salaam inayowakutanisha wadau kutoka
Mashirika mbalimbali yanayoshughulikia masuala ya jotoardhi kujadilia
njia zilizotumiwa na baadhi ya mashirika kufanikiwa kupata nishati hiyo
pamoja na uanishaji wa huduma tofauti zifanywazo na mashirika hayo
katika kulisaidia shirika la TGDC nchini Tanzania, mashirika
yaliyohudhuria warsha hiyo ni yakiwemo ya Benki ya Dunia (ESMAP), GDC la
Kenya, JICA la Japan, BGR la Ujerumani, ICEIDA la Iceland, Chuo cha
Umoja wa Mataifa kinachofundisha nishati ya Jotoardhi, TNO la Uholanzi
pamoja na Indonesia.
Mkurugenzi
wa Mipango na Maendeleo ya Biashara wa Shirika la Uendelezaji wa
Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Bwana Kato Kabaka akitoa mada
wakati wa Warsha ya siku mbili inayofanyika Jijini Dar es Salaam
inayowakutanisha wadau kutoka Mashirika mbalimbali yanayoshughulikia
masuala ya jotoardhi kujadilia njia zilizotumiwa na baadhi ya mashirika
kufanikiwa kupata nishati hiyo pamoja na uanishaji wa huduma tofauti
zifanywazo na mashirika hayo katika kulisaidia shirika la TGDC nchini
Tanzania, mashirika yaliyohudhuria warsha hiyo ni yakiwemo ya Benki ya
Dunia (ESMAP), GDC la Kenya, JICA la Japan, BGR la Ujerumani, ICEIDA la
Iceland, Chuo cha Umoja wa Mataifa kinachofundisha nishati ya Jotoardhi,
TNO la Uholanzi pamoja na Indonesia.
Mtaalamu
wa masuala ya nishati toka Benki Kuu ya Dunia (ESMAP) Bwana Thrainn
Fridriksson (aliyesimama mbele) akitoa mada wakati wa Warsha ya siku
mbili inayofanyika Jijini Dar es Salaam inayowakutanisha wadau kutoka
Mashirika mbalimbali yanayoshughulikia masuala ya jotoardhi kujadilia
njia zilizotumiwa na baadhi ya mashirika kufanikiwa kupata nishati hiyo
pamoja na uanishaji wa huduma tofauti zifanywazo na mashirika hayo
katika kulisaidia shirika la TGDC nchini Tanzania, mashirika
yaliyohudhuria warsha hiyo ni yakiwemo ya Benki ya Dunia (ESMAP), GDC la
Kenya, JICA la Japan, BGR la Ujerumani, ICEIDA la Iceland, Chuo cha
Umoja wa Mataifa kinachofundisha nishati ya Jotoardhi, TNO la Uholanzi
pamoja na Indonesia.
Mtaalam
wa masuala ya nishati ya jotoardhi toka Shirika la Pertamina Geothermal
Energy la nchini Indonesia Bwana Hendrik Kurniawan Sinaga (kulia)
akitoa mada wakati wa Warsha ya siku mbili inayofanyika Jijini Dar es
Salaam inayowakutanisha wadau kutoka Mashirika mbalimbali
yanayoshughulikia masuala ya jotoardhi kujadilia njia zilizotumiwa na
baadhi ya mashirika kufanikiwa kupata nishati hiyo pamoja na uanishaji
wa huduma tofauti zifanywazo na mashirika hayo katika kulisaidia shirika
la TGDC nchini Tanzania, mashirika yaliyohudhuria warsha hiyo ni
yakiwemo ya Benki ya Dunia (ESMAP), GDC la Kenya, JICA la Japan, BGR la
Ujerumani, ICEIDA la Iceland, Chuo cha Umoja wa Mataifa kinachofundisha
nishati ya Jotoardhi, TNO la Uholanzi pamoja na Indonesia. Kuhsoto ni
Mtaalam mwenzie wa masuala hayo Bwana Agus Zuhro.
Wadau
mbalimbali wa masuala ya nishati ya jotoardhi wakifuatilia
uwasilishwaji wa mada wakati wa Warsha ya siku mbili inayofanyika Jijini
Dar es Salaam inayowakutanisha wadau kutoka Mashirika mbalimbali
yanayoshughulikia masuala ya jotoardhi kujadilia njia zilizotumiwa na
baadhi ya mashirika kufanikiwa kupata nishati hiyo pamoja na uanishaji
wa huduma tofauti zifanywazo na mashirika hayo katika kulisaidia shirika
la TGDC nchini Tanzania, mashirika yaliyohudhuria warsha hiyo ni
yakiwemo ya Benki ya Dunia (ESMAP), GDC la Kenya, JICA la Japan, BGR la
Ujerumani, ICEIDA la Iceland, Chuo cha Umoja wa Mataifa kinachofundisha
nishati ya Jotoardhi, TNO la Uholanzi pamoja na Indonesia.
Wadau
mbalimbali wa masuala ya nishati ya jotoardhi wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya Warsha Jijini Dar es Salaam inayowakutanisha wadau
kutoka Mashirika mbalimbali yanayoshughulikia masuala ya jotoardhi
kujadilia njia zilizotumiwa na baadhi ya mashirika kufanikiwa kupata
nishati hiyo pamoja na uanishaji wa huduma tofauti zifanywazo na
mashirika hayo katika kulisaidia shirika la TGDC nchini Tanzania,
mashirika yaliyohudhuria warsha hiyo ni yakiwemo ya Benki ya Dunia
(ESMAP), GDC la Kenya, JICA la Japan, BGR la Ujerumani, ICEIDA la
Iceland, Chuo cha Umoja wa Mataifa kinachofundisha nishati ya Jotoardhi,
TNO la Uholanzi pamoja na Indonesia.
Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo.
Na Benedict Liwenga, Maelezo.
TGDC
imepewa lengo na Serikali la kuhakikisha kuwa inazalisha umeme wa
Megawati 200 na kuuingiza katika gridi ya Taifa kufikia mwaka 2020.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Meneja Mkuu wa Shirika la Uendelezaji Nishati ya
Jotoardhi Tanzania (TGDC) Mhandisi Boniface Njombe wakati wa warsha ya
siku mbili iliyofanyika Jijini Dar es Salaam ambayo iliwakutanisha wadau
kutoka Mashirika mbalimbali yanayoshughulikia masuala ya jotoardhi.
Mhandisi
Njombe alisema kuwa warsha hiyo ina lengo la kujadili njia mbalimbali
zilizotumiwa na baadhi ya mashirika hayo hadi kufanikiwa kupata nishati
hiyo ikiwemo uanishaji wa huduma tofauti zifanywazo na mashirika hayo
katika kulisaidia shirika la TGDC.
“Matokeo
ya warsha hii tuliyoifanya tumeweza kuwasiliana na wenzetu wa Benki ya
Duni (ESMAP) kwa kukusanya wataalam toka taasisi mbalimbali pamoja na
Mashirika mbalimbali ambayo yamewahi kufanya kazi hii ya utafutaji wa
nishati ya jotoardhi na lengo letu ni kutaka kufahamu njia ambazo
wenzetu walizitumia mpaka kufanikiwa ili na sisi tupate kujifunza”,
alisema Njombe.
Aidha,
aliongeza kuwa warsha hiyo itawezesha rasilimali chache zilizopo ziweze
kutumika ipasavyo katika kuleta matokeo ambayo TGDC inatarajia kuyapata
ili kuhakikisha kuwa lengo la upatikanaji wa nishati hiyo linafikiwa.
Sambamba
na warsha hiyo TGDC kupitia Wizara ya Nishati na Madini wametiliana
saini Mkataba wa makubaliano na Shirika linaloshughulikia nishati ya
Jotoardhi la nchini Iceland (ICEIDA) utakaoisadia Tanzania kupatiwa
vifaa mbalimbali vitakavyotumika katika maeneo ambayo jotoardhi
inasadikiwa kupatikana.
Utiaji
saini wa mkataba huo ulifanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja na kwa upande wa nchi ya
Iceland ulifanywa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ICEIDA Bwana
Engilbert Gudmundsson ukushuhudiwa na Meneja Mkuu wa Shirika la
Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) Mhandisi Boniface
Njombe na Wanasheria.
Akiongea
mara baada ya utiaji saini wa mkataba huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja alilishukuru shirika la
ICEIDA la nchini Iceland kwa mchango wao mkubwa wa kukubali kulisadia
shirika la TGDC ili kuhakikisha kuwa nishati hiyo inapatikana.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ICEIDA Bwana Engilbert Gudmundsson
ameahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza nishati
hiyo kwa kuendelea kutoa msaada wa kiufundi na vifaa vinavyotumika
katika utafutaji na uchimbaji wa nishati hiyo.
Warsha
hiyo ilihusisha wadau mbalimbali wakiwemo watu wa Benki ya Dunia
(ESMAP), GDC la Kenya, JICA la Japan, BGR la Ujerumani, ICEIDA la
Iceland, Chuo cha Umoja wa Mataifa kinachofundisha nishati ya Jotoardhi,
TNO la Uholanzi pamoja na Indonesia kwani hawa wote wameweza kufanikiwa
kuipata nishati hiyo, hivyo watatoa mchango mkubwa kuliwezesha shirika
la TGDC kupata mafanikio na hatimaye nishati hiyo kuweza kupatikana.
TGDC
NI Shirika Tanzu la Tanesco lililoanzishwa Desemba 2013 na kuanza rasmi
kufanya kazi zake mwezi Julai 2014 ili kuharakisha upatikanaji wa
nishati ya jotoardhi nchini.
No comments:
Post a Comment