Ukiachana
na hifadhi za taifa zitakazokufanya usichoke kutembelea miji na mikoa
mbali mbali ndani ya Tanzania, ni uwepo wa hoteli za kifahari zenye
utofauti wa kipekee na hoteli za nchi nyingine.
Jovago Tanzania,
wadau wanaohusika na masuala ya Hoteli kimataifa, wanapenda
kuorodhshea tano bora ya hoteli zilizo kwenye chati ya kukupa mandhari
zuri ya kiutalii wa kifahari hapa Tanzania.
1.Manta Resort-Pemba
Ni
hoteli ya kipekee yenye chumba cha kulala chini ya bahari ya Hindi.
Hoteli hii inakupa mandhari ya peponi utakapo jaribu kukaa ndani ya
chumba hicho, hii ni moja ya utalii ambao hutaweza kuusahau utembeleapo
eneo hili kisiwani Pemba.
2.Essque Zalu Zanzibar.
Essque
Zalu ipo Zanzibar, ni hoteli bora ya kimataifa yenye viwango vya huduma
kwa hali ya juu (five star). Ni sehemu pekee itakayokupa historia nzima
ya Zanzibar na fursa ya kutembelea fukwe kubwa nzuri zinazopatikana
maeneo ya Nungwi. Imejengwa kwa nakshi za kishwahili na za kisasa za
kuvutia.
3.Singita sasakwa Lodge –Serengeti
Eneo
lake ni zaidi ya ekari 300,000. Hoteli inavyumba vilivyojengwa kwa
mandhari ya kitamaduni za kiafrika, na uwezo wa kuona madhari ya
hifadhi ya taifa na mbuga ya wanyama Serengeti.
4.Park Hyatt –Zanzibar
Ni
hoteli inayokupa mandhari kamili na historia ya Zanzibar, hoteli
imezungukwa na bahari ya Hindi katika eneo la kihistoria la Stone town.
5.Hyatt Regency- Dar es Salaam.
Hii
ni hoteli yenye kiwango cha juu cha ubora wa kimataifa (Five star),
inauwezo wa kubeba watu wengi zaidi ya hoteli yoyote Dar es Salaam.
Inamandhari nzuri ya bahari ya Hindi, na vyumba vilivyojengwa kwa
teknolojia ya hali ya juu, inafaa zaidi kwa masuala ya makazi kwa
mikutano ya kibiashara pia inakupa fursa ya kutembelea sehemu tofauti
tofauti zilizo katikati ya mji wa Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment