JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YANCHI JESHI LA POLISI TANZANIA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 01.12.2015.
- WATU WATATU WAUAWA KATIKA MATUKIO MATATU TOFAUTI WILAYA ZA CHUNYA, RUNGWE NA MBARALI.
- WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA TUKIO LA AJALI JIJINI MBEYA.
- WATU WANNE WAKAMATWA NA SILAHA MBILI NA NYARA ZA SERIKALI WILAYANI CHUNYA.
- MTU MMOJA AKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI MENO YA TEMBO WILAYA YA MOMBA.
KATIKA LA TUKIO LA KWANZA.
MTU
MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IGUNDU AITWAE SIANA MWANDOLA [48], ALIUAWA
KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
KISHA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 29.11.2015 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KIJIJI
CHA IGUNDU,KATA YA CHOKAA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA.
INADAIWA
KUWA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI KULIPIZA KISASI KUTOKANA NA TUHUMA ZA
MAREHEMU KUHUSIKA KATIKA MAUAJI YA MWANAMKE MMOJA AITWAE ROZA KYUSA [63]
TAREHE 22.11.2015 MAJIRA YA SAA 02:00 USIKU. UPELELEZI UNAENDELEA ILI
KUWABAINI NA KUWAKAMATA WAHUSIKA WA TUKIO HILI
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI, BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA
WATU WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MZEE
MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA ILOLO, AITWAE BENARD BUJA [79], ALIKUTWA
AMEUAWA NYUMBANI KWAKE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA PANGA
SHINGONI NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA KWENYE SHAMBA MALI YA THOMAS
MWAMAKASI.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 30.11.2015 MAJIRA YA SAA 09:00HRS KIJIJI CHA ILOLO,KATA YA KIWIRA,TARAFA YA UKUKWE WILAYANI RUNGWE.
INADAIWA KUWA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI IMANI ZA KISHIRIKINA, KWANI MAREHEMU ALIKUWA ANATUHUMIWA KUWA NI MCHAWI KIJIJINI HAPO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHNA NA TABIA YA KUAMINI NA KUSADIKI
IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINASABABISHA MADHARA MAKUBWA KWA
JAMII IKIWA NI PAMOJA NA UPOTEVU WA NGUVU KAZI. AIDHA ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTU
MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IHENZANA AITWAE NIKO CHAULA [30], ALIUAWA KWA
KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
KISHA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 30.11.2015 MAJIRA YA SAA 17:00HRS KIJIJI CHA
MKUNYWA, KATA YA MADIBIRA,TARAFA YA RUJEWA, WILAYANI MBARALI.
INADAIWA
KUWA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI KULIPIZA KISASI KUTOKANA NA TUHUMA ZA
MAREHEMU KUHUSIKA KATIKA TUKIO LA KUPORA PIKIPIKI T.852 DAT AINA YA
YAMAHA MALI YA AIDAN WAYA [19], MKAZI WA ISOKO NA KUMJERUHI KWA KUMCHOMA
KISU TAREHE 29.11.2015 SAA 19:45HRS . UPELELEZI UNAENDELEA ILI
KUWABAINI NA KUWAKAMATA WAHUSIKA WA TUKIO HILI
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI, BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA WATU WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE.
KATIKA TUKIO LA NNE.
WATU
WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA SAMWEL SANGA [24], MKAZI WA UYOLE NA
AMANI SANGA [31], MKAZI WA UYOLE WALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI
WALILOKUWA WAKISAFIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.717 CFM AINA YA M/CANTER
ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA SAMWEL SANGA KUACHA NJIA, KUPINDUKA NA
KUSABABISHA VIFO VYAO.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 30.11.2015 MAJIRA YA SAA 06:30HRS ENEO LA UYOLE,KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA JIJINI MBEYA.
CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI. MILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO, IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA /KUFUATA SHERIA/ALAMA NA MICHORO YA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA TANO.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA BANANA – DSM
AITWAE LUKAS WAMBURA [38] MWENYE SHAHADA YA DHARURA YA KUSAFIRIA
AB-10044029 KWA KOSA LA KUKUTWA NA VIPANDE VINNE VYA MENO YADHANIWAYO
KUWA YA TEMBO VYENYE UZITO WA KILO 8.4 YENYE THAMANI YA DOLA ZA
KIMAREKANI 30,000, SAWA NA TSHS 64,140,000/=.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 30.11.2015 MAJIRA YA SAA 06:00HRS ENEO LA CUSTOM –
MPAKANI TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA.
INADAIWA
MTUHUMIWA ALIKUWA ANAVUKA MPAKA AKITOKEA NCHI JIRANI YA ZAMBIA KUINGIA
NCHINI NA MZIGO HUO ALIKUWA AMEUFICHA NDANI YA BEGI LAKE LA NGUO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA PINDI
WANAPOMTILIA SHAKA MTU/WATU ILI HATUA ZA HARAKA ZICHUKULIWE.
KATIKA TUKIO LA SITA.
JESHI
LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WANNE KWA KUKUTWA NA SILAHA MBILI PAMOJA
NA NYARA ZA SERIKALI AMBAO NI 1. MOHAMED HUSSEINNDILAVA [55], MKAZI WA
MKWAJUNI 2. NASSORA OMARY [65], MKAZI WA TABORA 3. MWANZA MTOKAMBALI
[39] MKAZI WA NJELENJE NA FRANK JONAS [32], MKAZI WA BITIMANYANGA.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 30.11.2015 SAA 21:00HRS KATIKA KIJIJI NA KATA YA KAPALALA,TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA.
INADAIWA
WATUHUMIWA WALIKUTWA NA SILAHA MOJA AINA YA RIFFLE 416 YENYE NAMBARI
C.6539833 NA GOBOLE MOJA LISILOKUWA NA NAMBA, PIA WALIKUTWA NA NYARA ZA
SERIKALI KICHWA KIMOJA CHA PAA, NYAMA YA PAA NA NYAMA YA SUNGURA VYOTE
VIKIWA NA THAMANI YA TSHS 1,176,000/=.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WAHALIFU WAKIWEMO
MAJANGILI KUZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO
ZICHUKULIWE MARA MOJA.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment