WITO WA KUTOA MAONI KUHUSU
SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA, SURA YA 410
_________________________
1.0 Utangulizi
Kama inavyofahamika,
Sheria ya Ununuzi wa Umma inayotumika sasa, Sura ya 410, ilitungwa na Bunge la
Jamhuri ya Muungano mwaka 2011 kwa lengo la kuweka mfumo wa kisheria na
kitaasisi wa usimamizi wa ununuzi wa umma.
Katika utekelezaji
wa Sheria hiyo, Serikali na taasisi zake zimebaini kasaro ambazo zimekuwa kikwazo katika utekelezaji
bora wa Sheria hiyo tangu ilipotungwa kwa mara ya kwanza mwaka 2001.
Kasoro
zimeendelea kuwepo hata baada ya Bunge kuifuta na kutungwa upya Sheria ya
Ununuzi wa Umma mwaka 2004. Kasoro hizo
ni pamoja na mlolongo mrefu na gharama nyingi katika mchakato wa ununuzi kabla
ya kufanya ununuzi unaokusudiwa.
2.0 Madhumuni ya Utafiti
Kwa kuzingatia
masharti ya kifungu cha 8(1) na (2) cha Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria
Tanzania, Sura ya 171, na Hadidu za Rejea zilizotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Tume inafanya utafiti kwa lengo la:
(i) Kubainisha upungufu katika utekelezaji wa Sheria
(ii)kubainisha madhara ya upungufu huo katika utekelezaji wa
Sheria kwa Serikali na taasisi zake
Baada ya kukamilisha
Utafiti, Tume itawasilisha Taarifa yenye Mapendekezo ya namna ya kuiboresha
Sheria ya Ununuzi wa Umma ili kuleta tija katika sekta ya Ununuzi wa Umma.
3.0
Maoni na Mapendekezo ya Wananchi
Ili kuwezesha kufanyika
kwa utafiti huo kikamilifu na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 10 (1) (2)
cha Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria, Sura ya 171, Tume inatoa wito kwa
watu binafsi, taasisi za Serikali na taasisi binafsi kushiriki katika kutoa
maoni na mapendekezo kuhusu masharti yaliyomo katika sheria ya Ununuzi wa Umma
mya mwaka 2011 na Kanuni za Ununuzi wa Umma zilizoandaliwa chini ya Sheria hiyo
kwa lengo la kuiboresha.
Maoni na
Mapendekezo yanaweza kuwa ya jumla au kuhusu masharti mahsusi ya Sheria au
mifumo ya kitaasisi iliyoundwa na Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa
kuzingatia mambo yafuatayo:
- (i) Misingi ya soko, pamoja na mabadiliko endelevu ya kisheria (Market fundamentals and dynamics of law)
- (ii) Hatua mbalimbali katika mchakato wa ununuzi wa bidhaa au huduma (procurement process and procedural and institutional requirements)
- (iii) Ulinganifu wa thamani ya fedha kwa bidhaa inayonunuliwa au huduma inayotolewa (Value for money)
- (iv) Mgongano unaojitokeza katika sheria zinazohusiana na ununuzi wa umma (Conflict of laws)
- (v) Athari za kibinadamu katika mchakato wa ununuzi kama vile rushwa, mgongano wa maslahi binafsi na ukosefu wa maadili (Human factors)
4.0 Muda wa Kupata Maoni/Mapendekezo
Ili kukamilisha
Utafiti huu mapema, Tume imeweka muda wa siku thelathini, kuanzia tarehe 15
Desemba, 2015 hadi tarehe 14 Januari 2016 za kupata maoni na mapendekezo kutoka
kwa Wananchi na taasisi husika.
5.0 Namna ya Kutuma Maoni/Mapendekezo
Maoni na
Mapendekezo yanaweza kuwasilishwa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kupitia
njia zifuatazo:
Anuani
ya barua
Katibu Mtendaji,
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania,
S.L.P. 3580,
DAR
ES SALAAM
Simu
ya Mezani
Simu: +255 22 2123533/2111387
Nukushi
Fax: 255 22 2123534
Barua
pepe
Mtandao wa Kijamii
Tovuti
Imetolewa
na:
Casmir
S. Kyuki
KATIBU MTENDAJI
No comments:
Post a Comment