Serikali kuendelea kuimarisha Sekta ya Uvuvi - LEKULE

Breaking

4 Dec 2015

Serikali kuendelea kuimarisha Sekta ya Uvuvi

uv1

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na uvuvi Bi Judith Mhina akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu mradi wa udhibiti wa uvuvi na maendeleo shirikishi Kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi “SWIOFISH” leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Bi Fatma Sobo.
uv2
Afisa Uvuvi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Bw. Silas William akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwainua wavuvi wadogo hapa nchini ili kushiriki katika kukuza uchumi wa Taifa. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Bi Fatma Sobo.mwisho kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na uvuvi Bi Judith Mhina.

uv3
Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi wakifuatalia mkutano wa Wizara hiyo na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.
uv4
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano kati yao na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambao pamoja na mambo mengine ulibainisha kuwa Serikali imejipanga kukomesha uvuvi haramu hapa nchini hasa kwa kutumia mabomu kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais,Wizara ya Mali asili na Utalii, Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya mambo ya Ndani na ile ya Katiba na Sheria.

No comments: