Sakata la Ufisadi Lililoibuliwa na Zitto Kabwe ......IKULU Yatoa Tamko,Yaitaka Stanbic Tanzania Ilipe Fidia ba Bilioni 13 Kwa Kufanya Udanganyifu - LEKULE

Breaking

1 Dec 2015

Sakata la Ufisadi Lililoibuliwa na Zitto Kabwe ......IKULU Yatoa Tamko,Yaitaka Stanbic Tanzania Ilipe Fidia ba Bilioni 13 Kwa Kufanya Udanganyifu


Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue akiongea na Waandishi wa Habari leo 01 Disemba, 2015 katika Ofisi ya Mawasiliano Ikulu kuhusu Tanzania kurejeshewa dola za Marekani milioni 7( sawa na bilioni 13) katika kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Jijini Uingereza dhidi ya Benki ya Stanbink Tanzania.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari leo 01 Disemba, 2015 katika Ofisi ya Mawasiliano Ikulu kuhusu Tanzania kurejeshewa dola za Marekani milioni 7( sawa na bilioni 13) katika kesi iliyofunguliwa katika Mahakama Jijini Uingereza dhidi ya Benki ya Stanbink Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bwana Assah Mwambene.

*********
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, leo amezungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam  kuhusiana na tuhuma zilizoelekezwa benki ya Stanbic Tanzania kuwa imetumika katika kufanya udanganyifu wa riba ya mkopo dola Milioni 600 (sawa  na Trioni 1.2 za kitanzania)  iliyopewa serikali ya Tanzania na Uingereza kupitia Kampuni ya Egma ya Tanzania.
 
Amesema serikali ya Tanzania iliipa kazi benk ya Stanbic bank iisadie kutafuta mkopo wa dola milioni 600 huko London  kwa ajili ya shughuli za maendeleo ambapo ada yake ilikuwa  asilimia 1.4% na fedha hiyo ilitakiwa ilipwe ndani ya miaka 7

Amesema kuwa pesa hiyo ilipofika Dar es Salaam, Stanbic Tanzania ambayo ni kampuni mama ya Standard Group iliongeza tena asilimia 1% kwa ajili ya wakala (kampuni ya Egma) wa standard bank wakati Standard Group na Serikali ya Tanzania hawakuhitaji wakala.

Sefue ameeleza kuwa,Stanbic Tanzania walimweka mtu hapa katikati, akachukua asilimia 1% ya mkopo wote ambayo ni dola milioni 6 ambazo hakustahili

Kwa mujibu wa Balozi Ombeni Sefue,udanganyifu wa utaratibu wa kumtafuta wakala wa ndani yaani Local Agent uliofanywa na benki ya Stanbic Tanzania ulibainika kutokana na uchunguzi uliofanywa na kampuni ya Serious Fraud Office ya London na kufungua kesi ambayo kampuni hiyo ilipata ushindi jana November 30, 2015 na kuiwezesha Tanzania kurejeshwa fedha hizo pamoja na faini.

Balozi Sefue amesema kuwa hivi sasa serikali inafanya uchunguzi kubaini ni kwa nini pesa hiyo ilipofika Dar es Salaam iliongezewa asilimia moja? Nani aliyeamua hivyo? na hiyo fedha ilienda wapi? maana hela hiyo iliwekwa katika akaunti na ndani ya siku chache ikatolewa yote bila benki kukusanya kodi ya zuio ambayo kwa mujibu wa sheria ya kodi ilipaswa kutozwa.
  


Msikilize Katibu mkuu kiongoze akiongelea sakata hilo


No comments: