Profesa Muhongo Kafuta Likizo Zote Za Wafanyakazi wa Tanesco.......Kawaagiza Pia Washushe Bei ya Umeme - LEKULE

Breaking

19 Dec 2015

Profesa Muhongo Kafuta Likizo Zote Za Wafanyakazi wa Tanesco.......Kawaagiza Pia Washushe Bei ya Umeme



Bei ya umeme inatarajia kushuka wakati wowote kuanzia sasa baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani )kuliagiza Shirika la Umeme (Tanesco), kushusha gharama za nishati hiyo.
Katika hatua nyingine, Waziri huyo amefuta likizo za wafanyakazi wa shirika hilo ili  washughulikie tatizo la umeme nchini huku akisisitiza kuwa hataki kusikia kukatika katika kwa umeme.
Profesa Muhongo alitoa maagizo hayo  jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta Gas Plant, ambapo alikwenda kwa ajili ya kukagua mitambo hiyo ili kuona kama yote inafanyakazi.
Akitoa maelezo ya mtambo huo, Meneja Mohamed Kisiwa alisema wana mitambo mitano na wana uwezo wa kuzalisha Megawati 42 kila saa.
Alisema gharama ya uzalishaji umeme kwa uniti moja ni Sh. 90 na wamekuwa wakiuza kwa Sh. 180 hadi 187.
Profesa Muhungo alisema kwa maelezo ya meneja  huyo, inaonyesha umeme wanaozalisha wanapata faida mara mbili hivyo alisema kuna uwezekano mkubwa wa kushusha  gharama za umeme.
Aliagiza maofisa wa wizara yake na wa shirika la Tanesco wakutane leo ili wajue umeme huo utashushwa kwa kiwango gani.
“Utauzaje umeme mara mbili ya gharama za uzalishaji,  tunataka kuwapunguzia wananchi bei ya umeme  na kwenye mkutano wetu wa kesho (leo) tutajadili  kupunguza bei ya umeme..haya mahesabu hayajakaa sawa maana unazalisha uniti moja kwa Sh. 90 na kuuza kwa Sh. 180 tutajadiliana mpunguze,” alisema.

Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipokea vifaa vya kuzuia kusikia sauti kuingia masikioni mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Mitambo ya Gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akizungumza na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam, Mohamed Kisiwa mara baada waziri wa Nishati na Madini kutembelea mitambo ya umeme wa gesi wa Tegeta jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipewa maelekezo na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta, Mohamed Kisiwa mara baada ya waziri huyo kutembelea mtambo huo bila kutoa taarifa na kuhoji baadhi ya matengenezo katika mtambo huo.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akitembezwa na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta Mohamed Kisiwa mara baada ya kutembelea mitambo ya Tegeta jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Mitambo ya Gesi iliyotembelewa na Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipewa maelekezo na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta, Mohamed Kisiwa jijini Dar es Salaam leo.



No comments: