MAHAKAMA
ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, imemhukumu askari polisi wa Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, G 9762 PC Daniel (24) kutumikia kifungo cha
maisha jela, baada ya kupatikana na makosa ya kubaka na kumlawiti mtoto
wa miaka 13.
Mbali
na kifungo hicho, mtuhumiwa huyo ameamriwa kulipa fidia ya Sh milioni 2
ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Hukumu
hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Said Mkasiwa
baada ya kukamilika ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa
mashtaka uliokuwa na mashahidi wanne.
“Mahakama
inatoa hukumu kwa mtuhumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 kwa kosa la
kubaka na kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti mtoto
na baadaye atalipa fidia ya Sh 2,000,000 ili iwe fundisho kwa wengine
wenye tabia kama hizo,” alisema Mkasiwa.
Katika
utetezi wake, mtuhumiwa kupitia kwa wakili wake ambaye alitajwa kwa
jina moja la Manzi, alidai kosa hilo ni la kwanza na ni kijana mdogo
ambaye ni nguvu kazi ya taifa, pia alifanya kosa hilo akiwa amelewa,
hivyo hakujua alichokuwa akikifanya.
Awali
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Elik Shija, alidai hakukuwa na
kumbukumbu za makosa ya nyuma dhidi ya mshtakiwa, hivyo aliiomba
mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa
wengine wenye tabia kama hiyo.
No comments:
Post a Comment