Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, amesema ameridhishwa na kasi ya utendaji kazi ambayo Rais Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim, wameanza nayo na kwamba ana imani kwa uchapakazi na uadilifu wao, wataivusha Tanzania na kuifikisha kwenye uchumi wa kati ambako serikali imejielekeza kufika.
Pinda
amesema yeye anaona kasi hiyo ya utendaji inayochukuliwa na serikali ya
awamu ya tano, ni sahihi na kinachohitajika ni kumuombea tu kwa Mungu.
Alitoa
kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana baada ya kufungua Kituo cha
Utamaduni cha China hapa nchini katika mahojiano maalum na waandishi wa
habari waliotaka kufahamu namna anavyoona kasi ya utendaji wa Serikali
ya Awamu ya Tano.
Alisema
kila rais anayeingia madarakani, lazima aingie na nguvu yake ya kufanya
kazi ambayo inaweza kujenga imani kwa wananchi wake na yeye anaona sawa
kasi hiyo aliyoingia nayo Dk. Magufuli.
“Unajua
kila rais anayeingia madarakani, lazima aje na nguvu yake ambayo
itajenga imani kwa wananchi, hivyo mimi naona ni sawa tu, kikubwa ni
kumuombea tu,” alisema Pinda kwa ufupi.
No comments:
Post a Comment